• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI JAFO AIPONGEZA KANDA YA MASHARIKI, AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA.

Posted on: August 7th, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (Mb) ameyapongeza maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki kwa maandalizi mazuri huku akitoa wito kwa wananchi kutunza mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaathiri sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima pamoja Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame wakati wakitembelea mabanda ya maonesho.

Waziri Jafo ametoa wito huo Agosti 8 mwaka huu wakati akizungumza na waandaishi wa habari baada ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea mabanda na vipando vya maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki vilivyopo eneo la Nanenane katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika Manispaa hiyo.

Waziri Jafo akimsikiliza Bw. Said Godfrey anaelezea mikakati, faida ya uzalishaji wa zao la mchikichi.

Waziri huyo amesema, ameridhishwa na maandalizi ya maonesho hayo kutokana na wadau wa sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi kuwa wamejiandaa vizuri katika kutoa elimu kwa wakulima ili iwasaidie, kwani kwa kufanya hivyo wametafsiri maelekezo ya Rais Samia ya kuwawezesha wakulima kielimu, zana na pamoja na fedha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akipokea zawadi kutoka kwa muwakilishi wa Meneja wa benki ya CRDB baada ya kutembelea banda hilo.

“...binafsi nimefarijika sana na maandalizi mazuri ya maonesho ya wakulima ya mwaka huu katika kanda hii...kwahiyo nimeona kwamba mmeendelea kuwa vinara wa maonesho mazuri ya Nanenane hapa Tanzania...” amesema Waziri Jafo.

Pamoja na pongezi hizo Mhe. Jafo bado amesisitiza suala zima la utunzaji mazingira kwa kuwa amesema kwa sehemu kubwa kilimo kinategemea mvua na kwamba uharibifu wa mazingira unasababisha athari mbalimbali ikiwemo ukame.

Amesema, Serikali imewekeza zaidi ya shilingi Bil. 214 kwa ajili ya kujenga marambo makubwa 114 hapa nchini kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na bila utunzaji wa mazingira kilimo hicho hakitafanikiwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amesema Kanda ya Mashariki inajukumu la kulinda mazingira kutokana na umuhimu wa mito inayopeleka maji katika bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere linalotarajia kuzalisha umeme zaidi ya Megawati 2000.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo baada ya kuwasili katika viwanja vya maonesho ya Nanenane 

Naye Bw. Said Godfrey kutoka Halmashauri ya ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani pwani, amewaeleza wananchi faida ya zao la mchikichi na kubainisha kuwa, koli moja la mchikichi unaweza kutoa lita tano za mafuta na mche huo mmoja unaweza kuzaa makoli zaidi ya 20 kwa mwaka, hivyo ameshauri wananchi wengine kujikita katika kilimo cha zao hilo la michikichi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima akiburudika pamoja na kikundi cha ngoma katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.