• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima ataka tarafa ya Nongwe kuwa kitovu cha mapinduzi ya kilimo.

Posted on: October 16th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa kijiji cha Lukinga Wilayani Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amedhamiria kukuza uchumi wa wilaya ya Gairo kupitia Tarafa ya Nongwe ambayo amesema itakuwa kitovu cha mapinduzi katika sekta ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Mhe. Malima amesema hayo Oktoba 15, 2023 wakati wa ziara yake ya siku moja katika Tarafa ya Nongwe Wilayani Gairo ziara iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero za wananchi na kujionea maeneo ya uzalishaji wa mazao ya chakula na  biashara likiwemo zao la parachichi na karafuu.

Mazao mengine ambayo amesema yanastawi na kutaka yawekewe kipaumbele katika uzalishaji ni pamoja na kahawa, maharagwe, viazi mviringo na ndizi ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo Bi. Sharifa Nabalang'anya na Afisa Kilimo wake kushauriana na kutoa elimu kwa wananchi ili kufikia lengo la kufanya mapinduzi ya kilimo katika Tarafa hiyo ya Nongwe kwa ajiri ya kuongeza kipato cha wananchi na kjongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo. 

Aidha, RC Malima amewaagiza Makatibu Tawala Wasaidizi sekta ya uzalishaji Dkt. Rozalia Rwegasira na Sekta ya miundombinu Mhandisi Ezron Kilamhama kushirikiana na wananchi wa Tarafa hiyo kuweka mikakati na mipango madhubuti ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Sharifa Nabalang'anya wakiangalia zao la kahawa.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amewashauri wakulima wa tarafa ya Nongwe kuacha kilimo cha mazoea ambacho hakina tija kwao badala yake amewaagiza wataalamu wa kilimo ngazi ya Mkoa na wilaya kutoa elimu ya kilimo cha kitaalam na kutenga mzeneo mahususi kwa ajiri ya uzalishaji wa mazao ya karafuu parachichi na kahawa.

Hata hivyo,  katika sehemu ya miundombinu ameutaka uongozi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kukamilisha haraka kazi ya kuboresha barabara yenye urefu wa kilometa 62.5 ikiwa 55.5 km ili kurahisisha usafirishaji wa mazao hayo mara yatakapokuwa yahitaji kupelekwa katika masoko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuongea na wananchi wa kijiji cha Lukinga ambacho Mhe. Adam Kighoma Ali Malima amekuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza kufika tangu kisajiriwe mwa 1995 amesema serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imelenga kuwafikia wananchi katika vijiji vyote bila kujali changamoto za barabara zilizopo huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa huo kuwa wa Mkuu wa Mkoa wa kwanza kufika katika kijiji hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe Jabir Makame wakati wakiangalia mazao mbalimbali yanayozalishwa Wilayani humo.

Nae, Mwakilishi wa Meneja wa TANROADS Mhandisi Goefrey Mutakubwa akijibu swali la Mkuu wa Mkoa lililohusu uboreshaji wa barabara ya Nongwe, amesema bajeti ya barabara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 serikali imetenga Tsh. milioni 915 kwa ajili ya ukarabati wa umbali wa kilometa 55.5 ili wananchi wa tarafa hiyo kuwa na uhakika wa usafiri kwa kipindi chote cha mwaka.

Akiwa katika kijiji cha Lukinga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amewaunga mkono vijana 42 waliokwenda mkoani  Njombe kupata mafunzo ya uzalishaji wa zao la Parachichi kwa lengo la kuja kuzalisha   kijijini hapo, hivyo amewapa gunia Nne za mbegu ya parachichi kama alama ya kuwaunga mkono vijana hao.

Viazi mviringo ni miongoni mwa mazao yanayolimwa Wilayani Gairo.

Lakini pia amewaahidi  kuwapa Tsh. 2,000 000/= ikiwa ni ghrama ya manunuzi ya mbegu walizootesha katika kitalu chao cha zao hilo na utaalamu huku pia akiahidi kukipa kikundi hicho cha vijana 42 fedha taslim 500,000 endapo wataazisha Akaunti ya benki kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha parachichi.

Hiki ni Kituo cha Afya Nongwe kilichopo Wilayani Gairo.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • Wizara ya Maji kutatua changamoto ya maji Morogoro

    July 02, 2025
  • RAS MOROGORO AFUNGA MAFUNZO YA PEPMIS, ATAKA UWAJIBIKAJI NA UAMINIFU

    June 28, 2025
  • RC MALIMA AMUUMA SIKIO DC MVOMERO, KUTUMIA BUSARA ZAIDI.

    June 27, 2025
  • RC MALIMA AENDELEA NA MAONO YA KUKUZA KILIMO MKOANI MOROGORO.

    June 27, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.