Utangulizi:
Wakati Tanganyika inapata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961, Mkoa wa Morogoro ilikuwa ni Sehemu ya Jimbo la Mashariki. Jimbo hilo lilijumuisha Mikoa ya sasa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Makao Makuu ya Jimbo yalikuwa Morogoro mjini ambapo pia Mkuu wa Jimbo aliweka makazi na Ofisi yake hapo. Mbunge wa kwaza Mwafrika kuongoza Jimbo hilo alikuwa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkoa wa Morogoro ulianza rasmi mwaka 1962 ukiwa na Wilaya tatu ambazo ni Morogoro Kilosa na Ulanga. Ni Mkoa wa pili kwa ukubwa hapa nchini kwa sasa ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora.
Mipaka na ukubwa wa Mkoa
Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa pili kwa ukubwa nchini ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora. Mkoa una eneo la kilometa za mraba 73,039. Eneo hili ni sawa na asilimia 7.7 ya eneo lote la Tanzania Bara, kati ya eneo hili Km2 2,240 ni eneo la maji. Mkoa umepakana na Mikoa ya Pwani na Lindi kwa upande wa Mashariki, Manyara na Tanga kwa upande wa Kaskazini na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mikoa ya Dodoma na Iringa na Upande wa Kusini unapakana na Mkoa wa Ruvuma na Njombe.
Hali ya Hewa
Mkoa hupata mvua mara mbili kwa mwaka. Mvua za vuli hunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi katikati ya mwezi Januari, na mvua za masika hunyesha katikati ya mwezi Februari na kuishia mwezi Mei mwishoni. Kiwango cha mvua ni kati ya milimita 600 katika sehemu za tambarare na milimita 1,200 katika miinuko. Hata hivyo, zipo sehemu zilizo na ukame ambazo hupata mvua chini ya milimita 600 kwa mwaka. Sehemu hizo ni pamoja na Tarafa za Gairo katika wilaya ya Gairo, Mamboya katika Wilaya ya Kilosa na Tarafa ya Ngerengere katika Wilaya ya Morogoro.
Utawala
Mkoa wa Morogoro kiutawala umegawanyika katika Wilaya saba ambazo ni Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga, Malinyi na Gairo.
Kufuatana na Muundo wa Serikali za Mitaa Mkoa una Halmashauri saba za Wilaya na Halmashauri ya Manispaa moja na halmashauri ya Mji wa Ifakara. Halmashauri za Wilaya ni pamoja na Kilosa, Gairo, Kilombero, Morogoro, Ulanga, Mvomero na Malinyi. Mkoa una majimbo ya Uchaguzi 11, Kata 214, Vijiji 673, Mitaa 295, vitongoji 3,452
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 idadi ya kaya za Mkoa wa Morogoro ni 489,688 zenye watu 3,197,104 ambapo kati yao wanawake ni 1, 617,235 sawa asilimia na wanaume ni 1,579,869. sawa na asilimia . Wastani wa idadi ya watu katika Kaya ni
WAKUU WA MKOA WA MOROGORO TANGU UHURU MWAKA 1961
NA. |
JINA |
KUANZIA |
KUISHIA |
1.
|
Mhe. Suleimani Kitundu (Mb)
|
1962
|
1963
|
2.
|
Mhe. Chifu Humbi Ziota (Mb)
|
1963
|
1964
|
3.
|
Mhe. Joseph Kapilima (Mb)
|
1964
|
1965
|
4.
|
Mhe. Edward Barongo (Mb)
|
1965
|
1968
|
5.
|
Mhe. Joseph Namata (Mb)
|
1968
|
1971
|
6.
|
Mhe. Anselm Lyanda (Mb)
|
1971
|
1976
|
7.
|
Mhe. Anna Margareth Abdallah (Mb)
|
1976
|
1982
|
8.
|
Mhe. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya (Mb)
|
1982
|
1986
|
9.
|
Mhe. John A. Mhavile (Mb)
|
1986
|
1990
|
10
|
Mhe. Mustafa Nyang’anyi (Mb)
|
1990
|
1991
|
11
|
Mhe. Yusufu Rajabu Makamba (Mb)
|
1991
|
1993
|
12
|
Mhe. Guntram Mkolokoti Aman Itatiro
|
1993
|
1995
|
13
|
Mhe. Ahmed Mayanja Katorogo Kiwanuka
|
1995
|
1996
|
14
|
Dkt. Lawrence Mtazama Gama (Mb)
|
1996
|
2000
|
15
|
Mhe. Alhaji Mussa Sekume kinanga Nkangaa
|
2000
|
2003
|
16
|
Mhe. Stephen Joshua Mashishanga (Mnec)
|
2003
|
2006
|
17
|
Mhe. Said bin Said Kalembo (Meja Jeneral Mstaafu)
|
2006
|
2009
|
18
|
Mhe. Issa Salehe Machibya
(Luteni Kanali Mstaafu) |
2009
|
2011
|
19
|
Mhe. Joel Nkaya Bendera
|
2011
|
2014
|
20
|
Mhe. Rajab Mtumwa Rutengwe
|
2014
|
2016
|
21
|
Mhe. Kebwe Steven Kebwe
|
2016
|
2019 |
22 | Mhe. Loata Erasto Olesanare | 2019 | 2021 |
23 | Mhe. Martine Reuben Shigela | 2021 | 2022 |
24 | Mhe. Fatma Abubakari Mwassa | 2022 | 2023 |
25 | Mhe. Adam Kighoma Malima | 2023 | hadi sasa |
MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WALIOONGOZA MKOA WA MOROGORO TANGU 1997
NA | JINA | KUANZIA | KUISHIA |
1 | Bi. Ndeshukurwa A. Sumari | 1997 | 2001 |
2 | Bw. Paul Chikira | 2001 | 2005 |
3 | Bw. Daud Mfwangavo | 2005 | 2006 |
4 | Bw. Godfrey Ngaleya | 2006 | 2009 |
5 | Bw. Hussein A. Kattanga | 2009 | 2010 |
6 | Bi. Mgeni S. Baruani | 2010 | 2012 |
7 | Bw. Eliya N. Ntandu | 2012 | 2016 |
8 | Dr. John S. Ndunguru | 2016 | 2017 |
9 | Bw. Clifford K. Tandali | 2017 | 2019 |
10 | Eng. Emmanuel N. M. Kalobelo | 2019 | 2021 |
11 | Bi. Mariam Mtunguja | 2021 | 2022 |
12 | Dr. Mussa Ali Mussa | 2022 | hadi sasa |
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.