Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) Mkoa wa Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Martine Shigela ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo imefanya ziara ya kutembelea Miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa na kwamba inaweza kutembelewa na Mwenge huo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikitembelea jengo la kituo Jumuishi (One stop Centre) la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. hapa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wanaangali vizimia moto (Fire Extinguisher) kwa ajili ya usalama wa jengo hilo.
Haya ni Majengo ya madarasa manne ya shule ya Sekondari ya Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambayo yatarajiwa kuwekewa jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru, 2021.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wametembelea miradi hiyo hivi karibuni katika Wilaya za Gairo, Kilosa na Morogoro na kuridhishwa na hatua ya miradi iliyofikiwa na kwamba wameridhika Mwenge kutembelea miradi hiyo mara utakapowasili Mkoani humo kuanzia Agosti 4 mwaka huu ukitokea Mkoani Iringa.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikikagua Mradi utakaopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2021 ambao ni nyumba ya wageni inayomilikiwa na mwekezaji mzawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela akimshauri jambo mmiliki wa nyumba hiyo ya wageni.
Ziara hiyo ni moja ya utaratibu wa Kamati hizo kwa kila mwaka Mwenge wa Uhuru unapokimbizwa kutangulia kufanya mapitio ya miradi yote kabla ya Mwenge kupokelewa ndani ya Mkoa ili kujiridhisha utekelezaji wake na kama miradi hiyo inakidhi vigezo vilivyowekwa na waratibu wa Mwenge wa Uhuru ngazi ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akionja Maji yaliosafishwa chumvi kwa mtambo wa maalum katika Mradi wa Maji wa Gairo. Kulia kwake ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Fortnatus Musilim.
Pamoja na kukiri ubora na hatua ya miradi waliyoitembelea kuwa kwenye kiwango bora, Mwenyekiti wa Kamati hiyo amewataka Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo kuendelea kusimamia ukamilishaji wa miradi ambayo haijakamilika na kumalizia mapungufu yaliyoonekana kwa baadhi ya miradi wakati wa ziara yao.
Moja ya majengo ya kituo cha Afya cha Mikumi wilayani Kilosa kilichotembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walipata fursa ya kutembelea jengo linalotarajiwa kuwa kiwanda cha kusindika Maziwa kinachomilikiwa na Jeshi la Magereza Morogoro ambacho kipo Mtego wa Simba wilayani Morogoro.
Mratibu wa mwenge Mkoa Bi. Winnifrida Madeba akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa mara tu baada ya kutembelea mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa kilichopo Mtego wa Simba ambacho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza Morogoro.
Mratibu huyo wa Mwenge Mkoa wa Morogoro Bi. Winnifrida Madeba wakati wote wa ziara hiyo amekuwa akisisitiza na kuwataka waratibu wa Mwenge ngazi ya Wilaya kuandaa nyaraka Sahihi za kila mradi na kupangwa inavyostahili ili kurahisisha wakimbiza mwenge mara watakapozihitaji wawapo katika mradi husika.
Mkoa wa Morogoro mwaka huu 2021 utaupokea Mwenge wa Uhuru Agosti 4 katika viwanja vya shule ya Msingi ya Ruaha Mbuyuni ukitokea Mkoa wa Iringa, utakimbizwa katika Wilaya zake zote saba za Mkoa huo hadi Agosti 10 na utakabidhi Mkoa wa Pwani Agosti 11 katika viwanja vya Shule ya Msingi Ubenalunch Wilayani Chalinze.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Hilary Sagala ambaye pia ni Afisa Tawala wa Wilaya hiyo akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela alipowasili Wilayani humo kukagua Miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa uhuru.
Haya ni Moja ya majengo katika Kituo cha Afya cha Malolo Wilayani Kilosa
Kauli Mbiu ya mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu inasema "TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU: ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI".
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.