Utangulizi:
Wakati Tanganyika inapata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961, Mkoa wa Morogoro ilikuwa ni Sehemu ya Jimbo la Mashariki. Jimbo hilo lilijumuisha Mikoa ya sasa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Makao Makuu ya Jimbo yalikuwa Morogoro mjini ambapo pia Mkuu wa Jimbo aliweka makazi na Ofisi yake hapo. Mbunge wa kwaza Mwafrika kuongoza Jimbo hilo alikuwa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkoa wa Morogoro ulianza rasmi mwaka 1962 ukiwa na Wilaya tatu ambazo ni Morogoro Kilosa na Ulanga. Ni Mkoa wa pili kwa ukubwa hapa nchini kwa sasa ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora.
Mipaka na ukubwa wa Mkoa
Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa pili kwa ukubwa nchini ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora. Mkoa una eneo la kilometa za mraba 73,039. Eneo hili ni sawa na asilimia 7.7 ya eneo lote la Tanzania Bara, kati ya eneo hili Km2 2,240 ni eneo la maji. Mkoa umepakana na Mikoa ya Pwani na Lindi kwa upande wa Mashariki, Manyara na Tanga kwa upande wa Kaskazini na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mikoa ya Dodoma na Iringa na Upande wa Kusini unapakana na Mkoa wa Ruvuma na Njombe.
Hali ya Hewa
Mkoa hupata mvua mara mbili kwa mwaka. Mvua za vuli hunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi katikati ya mwezi Januari, na mvua za masika hunyesha katikati ya mwezi Februari na kuishia mwezi Mei mwishoni. Kiwango cha mvua ni kati ya milimita 600 katika sehemu za tambarare na milimita 1,200 katika miinuko. Hata hivyo, zipo sehemu zilizo na ukame ambazo hupata mvua chini ya milimita 600 kwa mwaka. Sehemu hizo ni pamoja na Tarafa za Gairo katika wilaya ya Gairo, Mamboya katika Wilaya ya Kilosa na Tarafa ya Ngerengere katika Wilaya ya Morogoro.
Utawala
Mkoa wa Morogoro kiutawala umegawanyika katika Wilaya saba ambazo ni Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga, Malinyi na Gairo.
Kufuatana na Muundo wa Serikali za Mitaa Mkoa una Halmashauri saba za Wilaya na Halmashauri ya Manispaa moja na halmashauri ya Mji wa Ifakara. Halmashauri za Wilaya ni pamoja na Kilosa, Gairo, Kilombero, Morogoro, Ulanga, Mvomero na Malinyi. Mkoa una majimbo ya Uchaguzi 11, Kata 214, Vijiji 673, Mitaa 295, vitongoji 3,452
Idadi ya watu
Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya kaya za Mkoa wa Morogoro ni 489,688 zenye watu 2,218,492 ambapo kati yao wanawake ni 1, 125,190 sawa asilimia 50.7 na wanaume ni 1,093,302. sawa na asilimia 49. Wastani wa idadi ya watu katika Kaya ni 4:5
WAKUU WA MKOA WA MOROGORO TANGU UHURU MWAKA 1961
NA. |
JINA |
CHEO |
KUANZIA |
KUISHIA |
1.
|
Bw. Seleimani Kitundu (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1962
|
1963
|
2.
|
Chifu Humbi Ziota (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1963
|
1964
|
3.
|
Bw. Joseph Kapilima (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1964
|
1965
|
4.
|
Bw. Edward Barongo (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1965
|
1968
|
5.
|
Bw. Joseph Namata (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1968
|
1971
|
6.
|
Bw. Anselm Lyanda (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1971
|
1976
|
7.
|
Bibi Anna Margareth Abdallah (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1976
|
1982
|
8.
|
Bw. Crisant Majiyatanga Mzindakaya (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1982
|
1986
|
9.
|
Bw. Aaron Mhavile (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1986
|
1990
|
10
|
Bw. Mustafa Nyang’anyi (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1990
|
1991
|
11
|
Bw. Yusufu Rajabu Makamba (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1991
|
1993
|
12
|
Bwana Gutram Mkolokoti Aman Itatiro (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1993
|
1995
|
13
|
Dkt. Ahmed Mayanja Katorogo Kiwanuka
|
Mkuu wa Mkoa
|
1995
|
1996
|
14
|
Dkt. Lawrence Mtazama Gama (Mb)
|
Mkuu wa Mkoa
|
1996
|
2000
|
15
|
Alhaji Mussa Sekume kinanga Khangaa
|
Mkuu wa Mkoa
|
2000
|
2003
|
16
|
Bw. Stephen Joshua Mashishanga (Mnec)
|
Mkuu wa Mkoa
|
2003
|
2006
|
17
|
Said bin Said Kalembo (Meja Jeneral Mstaafu)
|
Mkuu wa Mkoa
|
2006
|
2009
|
18
|
Issa Salehe Machibwa
(Luteni Kanali Mstaafu) |
Mkuu wa Mkoa
|
2009
|
2010
|
19
|
Dkt. Joel Nkaya Bendera
|
Mkuu wa Mkoa
|
2010
|
2015
|
20
|
Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe
|
Mkuu wa Mkoa
|
2014
|
2015
|
21
|
Dkt. Kebwe Steven Kebwe
|
Mkuu wa Mkoa
|
2016
|
hadi sasa
|
Haki Miliki © 2018 Mkoa wa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa