• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

DC NGULI AIPONGEZA EXIM BANK.

Posted on: July 18th, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mhe. Judith Nguli ameipongeza Benki ya Exim kwa kuunga mkono juhudi za Serikali  Mkoani humo kwa kutoa vitanda 15 vya akina mama wajawazito ikiwa na lengo la kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitanda kwa akinamama hao wawapo katika vituo vya kutolea huduma za afya.


Mhe. Nguli ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima, ametoa Pongezi hizo  Julai 18, 2024 wakati akipokea vitanda hivyo 15 kutoka benki ya Exim  na kuvikabidhi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Best Magoma tukio lililofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.



Mkuu huyo wa Wilaya amesema, msaada huo uliotolewa kwa akina mama ni moja ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Mkoa wa Morogoro na wadau mbalimbali katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


"..Niwashukuru sana kwa namna ambavyo mnaunga mkono  juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za afya hasa kwa upande wa kina mama .." amesema Mhe. Judith.

Aidha, Mhe. Nguli ametoa wito kwa wadau wa taasisi na mashirika  mengine  Mkoani humo kushirikiana na Serikali pale wanapoguswa waweze kutoa huduma kwa jamii ili kuweza kuujenga Mkoa wa Morogoro na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Best Magoma amesema licha  ya kuendelea kupokea vifaa tiba mbalimbali kutoka Serikalini kuna upungufu wa vitanda  85 vya akina mama vya kujifungulia hivyo kupitia msaada huo kutoka Exim Banki vinaenda kupunguza adha ya ukosefu wa vitanda kwa vituo vya afya ambavyo havina vifaa hivyo.


Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Exim Bank Bw. Stanley Kafu amesema wanatambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya ndio maana nao wamefikia hatua ya kuunga mkono sekta hiyo kwa kutoa msaada huo huku akibainisha kuwa msaada huo sio mwisho wa kuiunga mkono Serikali bali wataendelea kutoa misaada mingine katika sekta mbalimbali   pale unapohitajika.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.