• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

DKT KIJANI ATOA POLE ZA MSIBA, ASEMA HUO NI MSIBA WA TAIFA

Posted on: May 23rd, 2024

Waziri wa viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametoa salamu za pole kwa ndugu jamaa, marafiki na watanzania wote kwa msiba mzito wa watu 11 waliopoteza Maisha na wengine wawili kujeruhiwa vibaya katika kiwanda cha Sukari cha Mtibwa cha Mkoani Morogoro baada ya kutokea hitilafu kiwandani hapo.


Dkt. Kijaji ametoa salamu hizo za pole leo Mei 23, 2024 mara baada ya kuwasili kiwandani hapo na kukagua eneo la tukio na kisha akazungumza na vyombo vya Habari kuhusu vifo vya ndugu hao 11 waliopoteza Maisha baada ya kuunguzwa na joto la mvuke baada ya bomba la kusafirishia mvuke huo (Boiler) kupasuka.


Akiwasilisha salamu hizo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Kijaji amesema Mhe. Rais anawapa pole sana na anawataka kuwa na subri katika kipindi hiki kigumu na kwamba huo ni msiba wa taifa.


 “……Mheshimiwa Rais anawapeni pole sana sana kwa ajali hii na anawaomba moyo wa Subira mnapopita katika kipindi hiki kigumu…huu ni msiba wa taifa tumetikisika kama taifa kwa ajali hii tulioipata…” amesema Dkt. Kijaji


Amesema watu 11 waliopoteza maisha watatu ni raia wa kigeni, na kwamba ajali hiyo imetokea wakati wanakamilisha azma ya Serikali ya Tanzania ya kuondoa changamoto ya upungufu wa sukari hapa nchini kuanzia mwaka 2025 kwa kwa makubaliano ya viwanda vyote vya sukari kuzalisha zaidi ambapo mpango huo kwa upande wa kiwanda cha mtibwa ulipangwa kuanza leo Mei 23,2024.


Akitoa salamu za pole ngazi ya Mkoa kwa wafiwa na jamii yote ya Kiwanda cha Mtibwa  Mkuu wa MKoa wa Morogoro Mhe. Adam Ali Kighoma Malima amesema gharama za kusafirisha miili ya marehem hao zitagharimiwa na Kiwanda hadi watakapowasitiri.


Aidha, Mhe. Adam Malima amebainisha kuwa kiwanda hakitafanya kazi ndani ya kiwanda hicho kwa siku tatu kwa ajili ya  maombolezo na kufanya uchunguzi wa miundombinu ya eneo lililotokea ajali endapo liko salama ili baada ya siku tatu kazi ziweze kuendelea.


Awali kiongea na vyombo vya Habari kuthibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro Shaban Marugujo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku Mwenyekiti wa makampuni ya super Group Seif A. Seif amewashukuru wananchi wote kwa kuonesha utulivu na mshikamano kwa kipindi chote maombolezo kwenye msiba huo mkubwa.




MWISHO



Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.