• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

DKT. SAMIA ATOA AGIZO.

Posted on: August 4th, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezitaka mamlaka za Mikoa na Wilaya hapa nchini kuhakikisha wanawasimamia vyema wenyeviti wa vijiji na watendaji wengine wa Serikali ngazi hiyo katika kutekeleza kazi zao kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni kwa lengo la kuepusha migogoro ya ardhi.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo leo Agosti 3, 2024 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya TUTUNZANE Wilayani Mvomero inayolenga kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Aidha, amewataka viongozi hao kutumia kampeni mbalimbali zakuleta suluhisho kwa njia ya Amani badala ya  kutoa matamko.

Amebainisha kuwa kilio kilichopo ni kwamba baadhi ya viongozi hao wa ngazi ya vijiji hawasimamii ipasavyo  serikali za vijiji, badala yake wanasubiri wananchi wakishaumizana uko ni rahisi kunyoosha mkono kupokea kuliko kuleta suluhu.

Aliwataka kuwasimamia wenyeviti wa vijiji waache kunyoosha mikono ,na walete  suluhu  za kweli na sheria lazima zifuatwe.

Rais Samia pia amemtaka kila Mwananchi kuheshimu Uhuru wa mwenzake kwa kila shughuli anayoifanya ikiwemo ya kilimo na ufugaji kwani wote wanategemeana  katika maisha ya kila siku.

Amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuwachukulia hatua wale wote watakaoingilia uhuru wa wenzao kwa manufaa binafsi.

" Kila mmoja aheshimu  mipaka ya mwenzie, kama unataka kulisha  mifugo kalishe kwenye   malisho sio kwenye mashamba, nanyie wakulima acheni kukata mifugo ya wenzenu" alisema.


Rais ameonesha kuridhishwa na kampeni hiyo ya kimkakati ya TUTUNZANE MVOMERO na amesema  Serikali itausimamia vema huku akiutaka uongozi wa Mkoa na wilaya ya Mvomero pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuusimamia mradi huo wa mfano kwa kutenga bajeti na kuwashirikisha wananchi kikamilifu.

Rais alitumia fursa ya mkutano huo kuwapatanisha wakulima na wafugaji kwa kuwataka wapeane mikono kama ishara ya kumaliza migogoro yao.


"Maugomvi mwisho leo na kwamba sasa wote mnakwenda kubadilika na kuingia kwenye mradi mkabadilike mlime mnaolimanna mnaofuga mkafuge, hakuna haja ya kugombana, mtumie mradi huu ,nyie wote mnatupa uhai na mnatupa vitoweo na vyakula" amesema.

Awali akizindua bwawa la umwagiliaji la Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza mawaziri wenye dhamana kuwa katika masuala yote ya ujenzi wa mabwawa, Maafisa Mazingira ngazi ya Taifa washirikishwe kikamilifu na kwamba suala la mazingira litiliwe maanani. .


" Hapa niweke msisitizo, nimeona kazi nzuri mnayofanya ya ujenzi wa mabwawa, tumieni maafisa Mazingira, suala la Mazingira litiliwe maanani, kwenye mabwawa, kiwandani na mashambani" alisema..


Aidha Rais Samia alisema Serikali itaendelea kulinda makundi yote na inapotokea imeegemea upande mmoja  wa wanyonge hivyo upande mwingine usione vibaya kwani serikali inasimamia na kutetea maslai ya makundi yote.


" ikitokea sukari imepanda hadi shilingi elfu saba lazima serikali isimame na wananchi kwani ndio walaji na chakula ndio kila kitu " alisema.


Alipongeza uongozi wa kiwanda cha Mtibwa kwa kutoa ajira zaidi ya 8000 kwa vijana na ajira 9000 kwa wakulima wa nje ambapo upanuzi ukikamilika zitafikia ajira ya watu 11,000


Hata hivyo Raisa Samia amesema Serikali katika kuthamini wawekezaji imeondoa msamaha wa kodi  shilingi bilioni 246  kwa viwanda 5  ambapo kwa  kiwanda  cha Mtibwa   pekee msamaha wa kodi ni  shilingi bilioni 80.9 .


"Nimeambiwa  uwekezaji wa kiwanda cha Mtibwa ni Dola milioni 155  na kwamba upanuzi wake ukikamilika utafikia dola milioni 805, huu sio uwekezaji mdogo, tulizoea kuona uwekezaji kama huu kwa wawekezaji wa nje lakini leo yupo huyu wa ndani " alisema.


Awali mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kiwanda cha Sukari cha Mtibwa Seif Ally Seif alisema wa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto ya umeme ambapo kati ya pampu 6 zinazopampu maji katika bwawa hilo ni mbili tu zinafanya kazi.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.