• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Dkt. Samia Atoa Wito kutunza miundombinu.

Posted on: August 2nd, 2024

Dkt. Samia Atoa Wito kutunza miundombinu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa  wananchi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kutunza  miundombinu  ya  Daraja la Berega kwa sababu daraja hilo limetumia gharama kubwa katika ujenzi wake hadi kukamilika  na kwa kufanya hivyo kutapelekea lidumu na kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Dkt. Samia ametoa wito huo Agosti 2, 2024 wakati akizindua Daraja la Berega linalounganisha wilaya za Gairo, Kilosa  mkoani Morogoro na Kilindi mkoani Tanga  ambapo hadi kukamilika kwake limetumia  zaidi ya shilingi Bilioni 7

Rais Samia amesema  uzinduzi wa daraja hilo umeondoa changamoto walizokuwa wakikumbana nazo wananchi wa maeneo hayo ambapo hapo mwazo walikuwa wanakwama kupita kwa sababu ya wingi wa maji, kushindwa kusafirisha mazao pia baadhi ya akina mama wajawazito wakishindwa kupita kwenda kupata huduma za kiafya katika hospitali ya Berega hivyo kusababisha hata vifo.

"... Ndugu zangu kujengewa daraja ni jambo moja, kutunzz daraja ni jambo lingine, kama mnavyojua daraja hili limetumia gharama nyingi sana naombeni tunzeni daraja.." amesisitiza Dkt. Samia

 Aidha Dkt. Samia ametoa wito kwa wananchi kutunza mazingira kando ya daraja ikiwemo kutokata miti ambayo husaidia kutotanuka mto na kuathiri daraja  hilo na kutochimba mchanga katikati ya daraja.

Katika Hatua nyingine Dkt. Samia amezindua hospitali ya Wilaya ya Gairo ambayo imegharimu shilingi Bilioni 4.8 ambapo imeenda kuondoa changamoto kwa Wananchi wa wilaya ya Gairo na  baadhi ya vijiji vya wilaya Kongwa Mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema kuzinduliwa kwa daraja hilo ni ishara ya upendo wa Mhe. Rais kwa watanzania bila ubaguzi, pia daraja hilo limepunguza adha kwa wanafunzi kutofika shuleni kutokana na maji kujaa na linaenda kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Tanga kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha mazao.

Nae mwananchi wa kijiji cha Berega  Bi. Violet Mwegoha amesema adha walizokuwa wakizipata kabla ya ujenzi wa Daraja hilo zikiwemo wagonjwa kushindwa kufika hospitali kwa wakati ambapo hupelekea vifo, pia kushindwa kusafirisha mazao kutokana na ujenzi huo adha hizo zimeondoka.

Ziara ya Mhe. Rais itaendelea Agosti 3, 2024 katika Wilaya ya Mvomero na Kilosa Mkoani Humo ambapo anatarajia pamoja na miradi mingine atazindua kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo katika Wilaya ya Kilosa.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.