• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Kiduku amshukuru RC kwa kutambua vipaji vya vijana, aahidi ushindi tena.

Posted on: September 11th, 2021

Mwanamasumbwi maarufu Mkoani Morogoro Twaha Ramadhan almaarufu kama Twaha  Kiduku amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela kwa kutambua na kuthamini vipaji  vya wanamichezo wa Mkoa wa Morogoro hususan vijana wanaochipukia kwenye tasnia mbalimbali za michezo Mkoani humo.

Twaha Kiduku akipokea cheti cha nidhamu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela.

Twaha Kiduku ametoa kauli hiyo Septemba 11 mwaka huu kwenye hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili yake kumpongeza baada ya ushindi wa pambano lake dhidi ya Abdallah Pazi almaarufu kama Dulla Mbabe iliyofanyika Cate Hoteli iliyopo Halmashauri ya Manispaa Morogoro Mkoani humo.

Twaha Kiduku ametoa shukurani na pongezi kwa Viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya na Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa huo Martine Shigela, Mkuu wa Wilaya hiyo Albert Msando, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mhe. Paschal Kihanga pamoja na wadau mbalimbali wa michezo ya ngumi Mkoani humo hii ikiwa ni baada ya kushinda shindano kati yake na Dulla Mbabe lililofanyika Agosti 20 Jijini Dar es Salaam.

“….Mimi nawaahidi ndugu zangu, mechi zozote  ambazo nitaletewa kwa sababu mimi huwa siogopi bondia  yoyote, mtu yeyote nikiletewa  wewe weka mzigo tupigane show show ….” amesema  kiduku.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni ishara ya mchango wake kwa Mwanamasumbwi Kiduku.

Meya wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro Mhe. Paschal Kihanga akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni ishara ya mchango kwa Mwanamasumbwi huyo.


Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni ishara ya mchango wake kwa Mwanamasumbwi Kiduku.

Baadhi ya Wadau wa Mchezo wa ngumi Mkoa wa Morogoro wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni ishara ya mchango wao kwa Mwanamasumbwi Kiduku.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na wadau hao wa Michezo Mkoani Morogoro wakishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ililenga pamoja na kumpongeza Mwanamasumbwi Twaha Kiduku lakini pia inakusudia kuwa mikakati mathubuti ya kuwaendeleza wanamasumbwi wote walioko ndani ya Mkoa huo akiwemo Twaha Kiduku.

MWISHO.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.