• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Michezo ya SHIMIWI yarejea tena

Posted on: October 20th, 2021

.

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imerejesha Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali – SHIMIWI iliyokuwa imesimamishwa tangu mwaka 2015.

Hayo yamebainishwa Oktoba 19 mwaka huu  na Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Daniel Zacharia alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Jamhuri uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakati wa maandalizi ya mashindano hayo.

Zacharia amebainisha sababu ya kusimamishwa kwa michezo hiyo kwa kipindi hicho cha miaka mitano kuwa inatokana na Serikali kuelekeza fedha iliyokuwa inatumika katika michezo hiyo kwenye shughuli za wa miradi ya maendeleo iliyokuwa ikitekelezwa wakati huo.

Katika hatua nyingine, Zacharia amebainisha lengo la mashindano ya SHIMIWI kwa watumishi wa Umma kuwa ni kuwajengea fursa wafanyakazi hao kufahamiana, kushirikiana, kujenga udugu na mazoea  ili  kurahisisha utendaji mzuri katika sehemu zao za kazi.

Aidha, amesema katika kipindi ambacho michezo hiyo ilisimama, Serikali ilielekeza watumishi wote wa Serikali kufanya mazoezi katika kila wiki ya kwanza ya mwezi ili kujenga Afya zao vizuri hususan kipindi hiki ambacho dunia nzima inakabiliwa na ugonjwa wa UVIKO – 19.

‘’Watumishi wetu kama watakuwa na Afya njema watashiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa taifa, kwa hiyo tunaishukuru Serikali na uongozi  mzima wa taifa hili’’ amesema Zacharia.

Awali akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amesema uzinduzi rasmi wa mashindano hayo ya SHIMIWI unatarajiwa kufanyika Oktoba 23 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro na mgeni Rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango.

Shigela amesema michezo mbalimbali inayotarajiwa kufanyika katika mashindano hayo ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mpira wa pete, netball, mashindano ya kukimbia  na michezo mingine.

Sambamba na hayo, Shigela ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro kushiriki na kushuhudia mashindano ya michezo hiyo na kuwataka wananchi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano, kuwaonesha upendo, kuwasaidia ili viongozi wake waweze kuvutiwa na ikiwapendeza mashindano yajayo tena yaweze kufanyika Mkoani humo.

 

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.