• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Morogoro Mkoa wenye fursa za uwekezaji, rasilimali Lukuki

Posted on: October 8th, 2021

Mkoa wa Morogoro umetajwa kuwa ni miongoni mwa Mikoa yenye fursa za uwekezaji na rasilimali za kutosha yakiwemo madini ya aina mbalimbali kutokana na mahali Mkoa ulipo na kwamba kinachohitajika ni mipango katika kuendeleza rasilimali hizo na kutumia vema fursa zilizopo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Baraza la Biashara la Mkoa huo lililofanyika Oktoba 9 mwaka huu  katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa huo lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya kibiashara kwa wakulima, wafanya biashara na wenye viwanda Mkoani humo.

Martine Shigela amesema Mkoa huo kijiografia uko sehemu sahihi kwa wawekezaji, wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda kwa kuwa uko katikati ya miundombinu muhimu ya usafirishaji kama Reli ya Kisasa, Reli ya kati na Reli ya TAZARA huku ikiwa ni kiunganishi cha barabara ziendazo mikoa ya nyanda za juu kusini, mikoa ya  kati na ya kaskazini.

Aidha, amebainisha kuwa Mkoa huo umesheheni fursa za kila sekta ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji, na kila aina ya madini hivyo jambo pekee ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi ni Wajumbe wa Baraza hilo la Biashara la Mkoa kutambua utajiri huo na kujipanga katika kuendeleza fursa hizo ili kuleta maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa jumla.

“Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa ambayo ina Big Pontential na sisi tuna pontential kubwa zaidi huenda kuliko maeneo mengine….mtu mwingine anatamani kuwa kwenye mazingira kama haya….” Alibainisha Martine Shigela.

“Kwa hiyo ni eneo ambalo kwa kweli tuone ni fursa kwetu na tulitumie vizuri, lakini pia ina kila aina ya mazao, ina kila aina ya uzalishaji ina kila aina ya fursa, ukisema utalii Morogoro ipo……ukisema madini ndo sisi tuna madini mengi zaidi” alibainisha Shigela.

Katika hatua nyingine, Martine Shigela alilitolea maelekezo suala la wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga waliojengewa vibanda katika Soko Kuu la Chifu Kingalu la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro jambo ambalo lililoibuka ndani ya kikao hicho akiwapa wamachinga hao wiki moja kurejea kwenye vibanda walivyojengewa lakini akiwatoa wasiwasi juu ya  mikataba wanayoidai kuwa watapewa ifakapo Januari mwakani na kwa muda huu hadi kipindi hicho wataendelea kufanya kazi zao bila kudaiwa chochote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Morogoro Mwazini Omary Muyanza pamoja na kukiri kuwa kikao cha mwaka huu kimekuwa na mafanikio makubwa kutokana na washiriki wake kutoka sekta mbalimbali kuongezeka, amewashauri wamachinga wa soko la Chifu kingalu kutekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa kurudi maeneo waliyotengewa kwani wanachokihitaji wao ndicho Serikali inakihitaji yaani kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabil Omari Makame alieleza umuhimu wa kikao hicho kuwa sekta binafsi ni Mshirika muhimu katika kuchochea maendeleo ya nchi na ndio maana Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaijali sekta hiyo kwa kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo changamoto ya ulipaji wa ushuru wa huduma.

kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Masele na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Omari Makame wakimsikiliza mwasilishaji wa mada wakati wa kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Masele yeye alijikita kuwataka wamachinga wa soko la Chifu Kingalu kwa kumueleza Mwenyekiti wao aliyeshiriki kikao hicho kukaa na wamachinga wenzake kusitisha mara moja zoezi la kuendelea kufanya biashara zao barabarani wakati wamejengewa vibanda vizuri huku akimsishi Mwenyekiti huyo anayesemekana kuwa ndiye kikwazo kikubwa kwa wamachinga kuhamia kwenye vibanda vyao kuachana na ushawishi huo usio na tija.

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya akisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wakati akifungua kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya huyo alimueleza mwenyekiti huyo kuelewe kuwa yeye amebeba mustakabali wa maisha ya watu na kuwashawishi wamachinga kutohamia kwenye vibanda walivyojengewa ni matumizi mabaya ya rasilimali fedha zilizotumika kuandaa eneo hilo na zoezi hilo halitaleta picha nzuri kwa viongozi wengi walioshiriki zoezi hilo siku ya uzinduzi wa vibanda hivyo akiwemo Waziri wa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Morogoro.

Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Morogoro.

Naye Meneja wa Kongani ya Kilombero inayoshughulikia mpango wa kuratibu kilimo biashara mikoa ya nyanda za juu kusini - SAGCOT Bw.John Mbaga ametaka  ushirikiano zaidi baina ya taasisi yake, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Serikali na sekta binafsi ili kufanya kazi kama timu hususan katika kutatua changamoto zinazojitokeza katika sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo lengo ni kuwasaidia wananchi kulima na kufuga kisasa hivyo kupata matokeo chanya.


Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano wa baraza la biashara 


MWISHO


 

  

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.