• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Morogoro yavuka lengo mapambano VVU/UKIMWI

Posted on: November 24th, 2023

Mkoa wa Morogoro umefikisha asilimia zaidi ya 95 ya lengo waliojiwekea la kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kutokana na Mkoa huo kuweka juhudi katika utoaji wa elimu ya kinga dhidi ya VVU kwa wananchi wake.

Hayo yamebainishwa Novemba 24, 2023 na Mhe. Adam Kighoma Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati akifungua wiki ya Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani humo. 

Mhe. Kighoma Malima amebainisha kuwa Mkoa huo uliweka malengo yake katika kuwafikia wananchi na kutoa Elimu dhidi ya kutokomeza VVU na UKIMWI kwa makundi mbalimbali ya jamii hususan Vijana.

Jitihada nyingine zilizotumika katika kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa huo ni pamoja na kutoa huduma ya ushauri na saha na upimaji wa hiari, matunzo na matibabu kwa watu waishio na VVU(WAVIU), hivyo juhudi hizo zimefanya Mkoa huo kuvuka lengo la 95 tatu.

Aidha, Mhe. Malima amesema Mkoa huo umevuka malengo ya tisini na tano tatu (95, 95, 95) hadi kufikia mwezi Septemba 2023 amabapo wananchi wanaotambua hali zao za Maambukizi ya VVU baada ya kupimwa ni asilimia 98.8, Wanaotumia dawa Kati ya watu waliogundulika kuwa na VVU ni asilimia 95 na kati ya watu wanaoishi na VVU ambao wanatumia dawa za kufubaza VVU – ARV nao wamefikia asilimia 95.8.

“...tisini na tano ya kwanza wananchi wanaotambua hali zao za Maambukizi ya VVU baada ya kupimwa ni asilimia 98.8, tisini na tano ya Pili Wanaotumia dawa Kati ya watu waliogundulika kuwa na VVU ni asilimia 95 na tisini tano ya tatu inaonyesha kuwa kati ya watu wanaoishi na VVU ambao wanatumia dawa za ARV wamefubaza VVU ni asilimia 95.8…” amesema Mkuu wa Mkoa.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amewashukuru wananchi wa Mkoa huo kwa kuwa na mwitikio chanya wa upimaji wa hiari ambapo kumekuwa na ongezeko la watu wanaopima VVU kila mwaka kutoka 226,213 kwa mwaka 2021, mpaka 292,731 kwa mwaka 2022 .

Hata hivyo amesema Mkoa umeendelea  kutoa huduma za upimaji wa VVU ambapo kwa mwaka huu kuanzia Januari hadi Septemba jumla ya watu 100162 walipimwa, kati yao wanawake 61665 na wanaume 38497 na waliogundulika na maambukizi ya VVU walikuwa 1,884 sawa na asilimia 2,  kati yao wanawake1,181 na wanaume ni 703. 

Akibainisha ratiba ya wiki ya maadhimisho hayo Mhe. Adama Malima amesema Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, yenye ujumbe usemao “Wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia”.  Kampeni hiyo itahitimishwa tarehe 10 Disemba, 2023.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano aliutoa hadi kufanikisha maadhimisho hayo. 

Naye mwakilishi wa Baraza la watu waishio na VVU (NACOPHA) Bw. Emanuel Msinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo za Afya na kutoa fursa kwa wananchi waishio na VVU kupata mikopo ambayo imewasaidia kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.