• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mufti wa Tanzania, RC Morogoro washiriki Mazishi ya Kadhi Mkuu, waumini waaswa kuzingatia Elimu.

Posted on: December 28th, 2024



Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zuberi Bin Ally na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima leo Disemba 28, 2024 wameshiriki mazishi ya aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Mussa Bolingo aliyefariki Dunia Disemba 27, 2024 saa moja jioni.

Akitoa salamu za msiba huo, Mufti Abubakar Zuberi pamoja na kumshukuru Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa  kugharimia Msiba huo amesema, wamempoteza Kiongozi mahili, mchapakazi na aliyekuwa anafanya kazi yake kwa umahili mkubwa na kuwataka waumini wa Mkoa huo kuwa na Subira.

“nini tunachoweza kusema, tumemkosa mtu, tumemkosa mwanachuoni, tumemkosa mchapakazi na tumemkosa mkombozi wa Mkoa wetu wa Morogoro” amesema Mufti Zuber.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewasisitiza waumini wa dini ya Kiislam kujiendeleza kielimu, elimu dunia na Elimu ya dini yao ili kuwa na maalifa katika kueneza ujumbe wa Mnyazi Mungu.

Aidha, naye ameungana na Mufti wa Tanzania kumshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushiriki kikamilifu kuwezesha na kufanikisha maziko ya Kadhi Mussa Bolingo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala ambaye katika salam zake za pole aliwataka waumini wa Kiislam na wote walioshiriki mazishi hayo  kuenzi mema ya Kadhi huyo, alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amegharimia chakula kwa ajili ya waombolezaji, sanda, usafiri na mambo mengine yote muhimu yaliyohitajika katika kufanikisha mazishi ya Kadhi Bolingo.

Pamoja na salamu hizo, Sheikh wa Mkoa wa Morogoro Twaha Kilango amebainisha kuwa Marehemu Mussa Bolingo aliifanya kazi yake kwa weledi mkubwa na kwamba katika uongozi wake hadi umauti unamkuta hajawahi kupewa malalamiko ya kazi yake ya Ukadhi aliyokuwa anaifanya ndani ya eneo lake la Mkoa wa Morogoro.

Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdul Azizi Abood akitoa salamu za pole amesema, Kadhi sheikh Mussa Bolingo alikuwa mpenda maendeleo hususan huduma za kijamii ikiwemo Afya na Elimu ambapo ameahidi kutekeleza ahadi aliyokuwa amemwahidi Marehem ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa ahanati aliyokuwa ameianzisha.

Marehemu Sheikh Mussa Bolingo amezikwa Disemba 28, 2024 baada ya swala ya alasiri katika eneo la msikiti wa Luqman uliopo Kihonda kwa Chambo Manispaa ya Morogoro.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.