Mwenge wa uhuru 2025 umeendelea kukimbizwa Mkoani Morogoro na kupitia miradi kadha wa kadha ya maendeleo huku ukiwa na kaulimbiu inayosema "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu" huku ukiweka bayana Tunu kuu Nne zilizoachwa na waasisi wa Taifa hili.
Kiongozi wa mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi akiwa Wilayani Kilosa Aprili 18, 2025 akitoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru kwa wananchi wa Wilaya hiyo amezitaja baadhi ya tunu zilizoasisiwa na viongozi waTaifa hili ambazo zinaendelea kuchochea maendeleo ya Taifa letu.
Moja ya tunu hizo ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo yaliondoa utawala wa kisultan na kumpa heshima Mzanzibar, pili Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa taifa la Tanzania.
Tunu nyingine zilizobainishwa ni azimio la Arusha la mwaka 1967 linalosisitiza Siasa za Ujamaa na Kujitegemea na Nne sera Madhubuti za ndani na Nje ambazo hazifungamana na upande wowote.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa amewataka wananchi kushiriki kikamilifu Uchaguzi Mkuu 1wa mwaka huu kwa Amani na Utulivu.
Mwenge wa Uhuru unategemea kukamilisha mbio zake mkoani Morogoro hapo kesho Aprili 19, 2025 na kuukabidhi mwenge huo Mkoa wa Dodoma tarehe 20/4/2025.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.