• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mwenge wa Uhuru waipongeza Malinyi utekelezaji miradi ya maendeleo.

Posted on: May 8th, 2023

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndg. Abdallah Shaib Kaim amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa utekelezaji mzuri na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe.  Sebastian Waryuba amepokea Mwenge wa Uhuru pamoja na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakitokea Wilayani kwa ajili ya kuendelea kukimbizwa katika Halmashauri hiyo.

Ndg. Shaib ametoa pongezi hizo Mei 8 mwaka huu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya msingi ya Itete Njiwa iliyopo Wilayani humo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 ndg. Abdallah Shaib Kaim ameongoza zoezi la upandaji miti katika enelo la shule ya Sekondari Njiwa iliyopo Wilayani Malinyi.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge amesema amejiridhisha na nyaraka mbalimbali za miradi ya maendeleo kwa kuzipitia kwa umakini ili kujiridhisha na taarifa zilizomo, ubora wake na vigezo vya mradi na kubaini kuwa miradi hiyo imekidhi vigezo vya kuwekewa jiwe la msingi, kuonwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

“...nitumie fursa hii kuwapongeza wote, Mkuu wa Wilaya, Mbunge, viongozi wa Halmashauri, mmefanya vizuri, mradi umekidhi vigezo... hivyo Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 umeridhishwa na taarifa za mradi.


Aidha, Ndg. Shaib amewahimiza wakazi wa Itete  na Tanzania kwa ujumla kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa rushwa ni adui wa haki na wa maendeleo ya nchi hivyo hawanabudi kushikamana kupiga vita Rushwa.


Awali, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kipenyo Bi. Restuta Kumpindi akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje katika Zahanati ya kijiji hicho, amesema ujenzi huo uliogharimu zaidi ya Tsh. milioni 81,389,240 utasaidia wananchi 4099 kupata huduma za matibabu katika vijiji vya jirani, kwani wakazi hao walikuwa wanatembea umbali wa kilometa tano kufuata huduma ya Afya kituo cha Afya Mtimbila.


Nae, Mbunge wa jimbo la Malinyi Mhe. Antipasi Mgungusi amempongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.


Mwenge wa Uhuru unatarajia kuendelea kukimbizwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara kesho Mei 9 mwaka huu.



MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.