• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mwenyekiti wa UWT Taifa awaonya wanaotumia majanga kutangaza Siasa

Posted on: April 23rd, 2024

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bi. Mary Chatanda amewaonya Wanasiasa wanaotumia majanga yatokanayo na mafuriko ya mvua kutumika kama fursa ya kufanya kampeni za kisiasa katika maeneo yao na badala yake amewataka watoe misaada hiyo kama pole kwa waathirika.



Bi. Mary amebainisha hayo aprili 23, Mwaka huu wakati alipotembelea kata ya Lipangalala katika Halmashauri ya Ifakara Mji Wilayani Kilombero kutoa pole na misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko yatokanayo na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilayani humo.

Aidha, Bi. Mary amesema kuwa wananchi wanahitaji faraja na misaada katika kipindi hiki kigumu na sio kueneza siasa kupitia misaada hiyo kwani kufanya hayo hayaleti picha nzuri na si uungwana ndani ya Taifa letu.

"...wapo baadhi ya watu sasa wanataka kutumia majanga haya katika masuala ya kisiasa.... hawaji kutoa misaada bali kuja kupiga porojo za Siasa... "amesema Bi. Mary Chatanda.

Sambamba na hilo, Mwenyekiti huyo ametoa pole na misaada mbalimbali ikiwemo nguo za watoto, vitenge, chakula na vyombo vya nyumbani kwa waathirika ili kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwafariji wananchi wanaoathiriwa na majanga hayo hapa nchini.

Pia, amesema baada ya mvua nyingi kupungua serikali itatoa mbegu za mazao za muda mfupi hususan maeneo yaliyoathiriwa kwa ajili ya kupunguza tatizo la chakula na kutoa mikopo ya 10% kwa wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu kwani Halmashauri zimeshaelekezwa kuweka utaratibu mzuri wa kupata mikopo hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wadau mbalimbali wa sekta binafsi na umma kuendelea kutoa misaada Mkoani humo kwani mafuriko yamekuwa yakiukumba Mkoa huo kwa nyakati tofauti tofauti na kuziomba Halmashauri za Ulanga na Malinyi kuwa wavumilivu na wasikivu wakati serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan sikivu ikijiandaa kuwafikia nao kwani  Mkoa huo ni mkubwa na mahitaji ni mengi.

Kwa niaba ya wananchi wenzake Bw. Hamis Saidi Konga mkazi wa kata ya Lipangalala, ameishukuru serikali kwa kuwajali kwani mafuriko hayo yameleta athari kubwa kwa makazi yao kama baadhi ya nyumba kubomoka, kuharibika kwa mazao na hata vifo vya watu wawili na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kutoa misaada kwani mahitaji bado yanahitajika kwa kiasi kikubwa.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.