Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amebainisha misingi mikuu mitatu inayomwongoza katika kuliongoza Taifa kuwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau katika maamuzi, uamuzi unaozingatia ushaidi na tafiti pamoja na kutanguliza mbele maslahi mapana ya Taifa lenyewe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan amebainisha hayo wakati akitunukiwa Shahada ya Udakatari wa heshima katika Uongozi na Chuo Kikuu cha Mzumbe kwenye Sherehe za mahafali ya 23 ya chuo hicho kilichopo Mkoani Morogoro.
Amesema, uongozi wake unatekeleza majukumu kwa kuzingatia taratibu na misingi ambayo huwezesha Serikali kufanya maamuzi sahihi na kuweza kutatua changamoto zinazowakabili Watanzania misingi hiyo ni ushirikishwaji wa wadau katika kufanya maamuzi, kufanya maamuzi kwa kutumia ushahidi na tafiti pamoja na kutekeleza kazi zote kwa kuzingatia malsahi ya Watanzania.
"..Mtindo wangu wa uongozi umejengeka juu ya misingi mikuu 3 ambayo ni ushirikishwaji, kutumia ushahidi katika maamuzi na kutanguliza maslahi ya Taifa.." Amesisitiza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Mhe. Rais ametoa wito kwa vingozi wa Serikali wa ngazi zote kutekeleza majukumu na wajibu wao ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuwaletea maendeleo yao na kuwatumikia Watanzania kwa moyo mmoja.
Sambamba na hayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na kuupongeza uongozi wa chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kutumia fedha za ndani kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya chuo hicho na kutatua changamoto nyingi zinazowakabili wanafunzi wa chuo hicho kwa kutumia fedha hizo za ndani.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.