• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RAS Morogoro afunga rasmi UMITASHUMTA, atoa agizo kwa wakurugenzi

Posted on: May 30th, 2023

RAS Morogoro afunga rasmi UMITASHUMTA, atoa agizo kwa wakurugenzi.

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa amefunga mashindano ya Umoja wa michezo kwa shule za msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ngazi ya Mkoa huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kusaidia timu zao zinazoshiriki mashindano hayo kwa kuwapatia vifaa vya michezo pamoja na kutoa michango ya ushiriki.

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa akitoa zawadi ya makombe kwa washindi wa michezo mbalimbali katika mashindano ya Umitashumta kwa Mkoa wa Morogoro.

Hafla hiyo ya ufungaji wa mashindano hayo imefanyika Mei 29 mwaka huu katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Morogoro iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambapo Halmashauri zote 9 za Mkoa huo zimeshiriki kwa kutoa wanamichezo.

Dkt. Mussa amesema kuwa Wakurugenzi wanajukumu la kusaidia wanamichezo wao kwa kutoa michango ikiwemo fedha za ushiriki na vifaa vya michezo kwa mashindano yajayo hivyo wakurugenzi wajipange kikamilifu.

Dkt. Mussa Ali Mussa akizungumza na washiriki wa mashindano ya Umitashumta ngazi ya Mkoa pamoja na Viongozi wao wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo.

“...lakini mbaya zaidi hata hao wanafunzi wanaokuja kuwakilisha halmashauri zenu mmeshindwa kuwapa sare nzuri sasa mimi niwaambieni hili sitaki kuliona tena kwenye michezo ijayo...” amesema Dkt. Mussa.

Aidha, Katibu Tawala huyo amesema michezo ina faida nyingi sio kuimarisha afya bali hupanua uwezo wa akili kufikiri, pamoja na kupunguza matukio ya kiharifu kwa sababu watu watatumia muda mwingi kwenye michezo kuliko kukaa  vijiweni bila kazi.

Sambamba na hilo Dkt. Mussa amewatakia kila la heri wanamichezo waliochaguliwa kuuwakilisha Mkoa  katika Mashindano hayo ngazi ya Taifa yatakayofanyika Juni 2, 2023 Mkoani Tabora na kuahidi kuandaa zawadi endapo timu hiyo itafanya vizuri katika mashindano hayo.

Washiriki kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wakionesha kipaji chao cha kuimba mbele ya mgeni rasmi.

Awali, Afisa Michezo Mkoa wa Morogoro Bi. Grace Njau amesema mashindano hayo yamewakutanisha wanamichezo 938 kutoka Halmashauri za Mkoa huo wakiwemo wavulana 453, wasichana 485 ambao wameshiriki michezo mbalimbali ikiwemo michezo ya riadha, mpira wa miguu, netiboli, mpira wa wavu, kwaya, na muziki.

Afisa michezo Mkoa wa Morogoro Bi. Grace Njau akitoa taarifa fupi ya mashindano ya Umitashumta kwa Mkoa wa Morogoro.

Bi. Grace ameongeza kuwa mashindano ya mwaka jana Mkoa wa Morogoro ulishika nafasi ya tano kitaifa, pia ulipata Medali nne katika mashindano ya Afrika.

Mashindano hayo kwa mwaka huu yanaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “Uimarishaji wa miundombinu ya elimu nchini ni chachu ya taaluma, sanaa na michezo”. Jumla ya wanamichezo 102 wamechaguliwa kuuwakilisha Mkoa katika mashindano hayo ya UMITASHUMTA ngazi ya taifa Mkoani Tabora ambayo yataanza Juni 2 mwaka huu.

MWISHO. 

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.