• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RAS Morogoro azionya NGOs.

Posted on: July 8th, 2024


Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa amekemea vikali baadhi ya mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani humo kuwa na tabia ya kutafuta maslahi binafsi badala ya mashirika hayo kuwaletea wananchi maendeleo yao.

Dkt. Musaa ametoa kauli hiyo  Julai 8, 2024 wakati akifungua semina ya mafunzo ya kuyajengea uwezo mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Amesema, lengo la kuazishwa kwa mashirika hayo yasiyo ya kiserikali ni kuisaidia jamii, hivyo amezitaka kila NGOs mkoani humo kutekeleza  lengo la kuanzishwa kwake badala ya kujinufaisha.

Akibainisha zaidi Dkt. Mussa amesema, baadhi ya mashirika hayo yakipata fedha kutoka Serikalini huwa hawatimizi malengo waliyojiwekea ambapo ni kinyume na taratibu walizojiwekea.

"....Hizi NGOs huwa zinatumika vibaya, yale mambo wanayotakiwa wayafanye huwa hawayafanyi, hizi NGOs badaya ya kuwa msaada kwa yale makundi ambayo yamekusudiwa bali hujisaidia wao wenyewe..." amesisitiza Dkt. Mussa

Kwa sababu hiyo, Dkt. Mussa ameonya vikali kuwa NGOs yoyote Mkoani humo itakayokiuka na kwenda kinyume na malengo yake ya uazishwaji itachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.

Kwa upande Wake Bi. Vidah Malle kutoka Wizara ya fedha amesema mafunzo hayo yataenda kuyajengea uwezo mashirika yasio ya kiserikali katika utekelezaji wa majukumu yao, kufahamu sheria na miongozo mbalimbali, kufahamu kuandaa bajeti nzima ya serikali na mchango wao katika bajeti hiyo.

Naye kiongozi wa Baraza la Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (Nacongo) Mkoa wa Morogoro Bw. Otanamusu Nicholaus  amesema mafunzo waliyoyapata yatasaidia kuyajenga mashirika hayo katika ngazi zote Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Amesema, lengo la mashirika  hayo ni kusaidia jamii  hivyo ameyataka mashirika yanayopata fedha kutoka Serikalini kuacha  tabia ya kutafuta maslahi binafsi badala yake fedha hizo zitumike kuiletea jamii maendeleo.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.