• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AAGIZA MAMA LISHE KUPEWA MIKOPO YA 10%.

Posted on: July 12th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Emmanuel Mkongo kutoa mikopo ya 10% kwa kikundi cha Mama Lishe chenye idadi ya watu 32 walio jisajili katika Kituo cha Treni ya kisasa cha Manispaa ya Morogoro ili kupata mtaji wa kuendesha biashara zao.

Adam Malima ametoa agizo hilo Julai 12, Mwaka huu wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya treni ya mwendo kasi - SGR  hususan ya kituo cha treni hiyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwa ni maandalizi ya treni ya SGR kuanza safari yake ya kutoa huduma kwa wananchi  kutoka Dar es Salaam – Morogoro na Dodoma ifikapo Julai 25 mwaka huu.

Mhe. Adam Malima amesema reli hiyo ya kiwango cha kisasa itasaidia kukuza uchumi wa Mkoa huo na nchi kwa ujumla, hivyo wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo kufanya shughuli za kiuchumi zikiwemo biashara, utalii na kilimo kwa maslahi mapana ya jamii na taifa.

Akifafanua zaidi kuhusu agizo la mikopo kwa akinamama hao amewataka kila mmoja kuweka bajeti ya kiasi anachotaka kukopa na  wakishapata jumla ya kiasi chote waende kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro wakubaliane ili waweze kukopeshwa.

"... kaeni mkubaliane muunde kikundi kimoja mkienda Halmashauri mtaandikishwa mkikubaliana nendeni mkachukue mitaji ya 10% mboreshe biashara zenu..." amesema Mhe. Malima

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amewashauri wananchi hususan Mama lishe wanapochukua fedha za mkopo kutoka Halmashauri husika wajikite kuzalisha na kuwa waaminifu kurudisha fedha hizo ili kupewa watu wengine wenye uhitaji.

Katika hatua nyingine Mhe. Malima ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kujenga vituo vya Maafisa usafirishaji wakiwemo Boda boda 250, madereva teksi 50 na waendesha pikipiki za magurudumu matatu maarufu kama Bajaji 150 pamoja na kujenga eneo la Mama lishe ambao idadi yao ni 32 ili kuwa na maeneo maalum ya kufanyia kazi.

Kwa upande wake, Bi. Jamila Mbarouk, Mkuu wa Kitengo cha habari cha Shirika la reli Tanzania (TRC) amesema maafisa hao na Mama lishe hao wamesajiliwa na kutambuliwa rasmi na TRC wakishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kwa lengo la kuwasafirisha abiria na kutoa huduma ya chakula abiria watakaposhuka kituoni hapo na kujipatia kipato.

Naye, Mwenyekiti wa kikundi cha Mama lishe Bi. Happiness Samuel Chilingo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ujio wake huku akitoa ombi la kupewa sehemu ya kufanyia biashara yao ya chakula.  

Kwa upande wao Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwakilishwa na Bw. Emanuel Jacob wamemuomba Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Kighoma Malima kutengenezewa barabara, sehemu ya kupaki pikipiki na kujengewa choo maombi ambayo yote ni ya muhimu, ameyapokea na kuwaahidi kuyafanyia kazi.


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.