• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AAGIZA WAAJIRI KUUNDA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

Posted on: May 1st, 2024

RC MALIMA AAGIZA WAAJIRI KUUNDA VYAMA VYA WAFANYAKAZI


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima  amewaagiza waajiri wote wa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka mazingira wezeshi ya kuunda vyama vya wafanyakazi na kuacha kuzoofisha vyama hivyo ndani ya taasisi zao ili kusaidia kutatua changamoto za wafanyakazi na kupunguza migogoro ya kikazi.

Adam Kighoma Malima ametoa Wito huo May 1, 2024 wakati akihutubia siku ya wafanyakazi ambapo  kwa Mkoa wa Morogoro maadhimisho hayo yamefanyika Halmashauri ya Mji Ifakara, yakiwa na kaulimbiu isemayo "nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga juu ya hali ngumu ya maisha".

Mkuu huyo wa Mkoa amesema, Serikali ngazi ya Mkoa na Serikali Kuu zitaendelea kushirikiana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuweka makubaliano ya pamoja ili kuhakikisha vyama hivyo vinawasaidia katika kupata hakim zao na maslai yao kikamilifu.

“……Nitumie fursa hii kwa waajiri wote wa sekta ya umma na sekata binafsi kuwataka kuweka mazingira wezeshi ya kuwepo kwa vyama vya wafanyakazi na kuacha tabia ya kuvizoofisha vyama hivyo kwenye taasisi zenu..” amesema Adam Malima.

Aidha Mhe. Malima ameiagiza ofisi ya Afisa kazi Mkoa na Afya (OSHA) kufuatilia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kujiridhisha kikamilifu mikataba ya wafanyakazi endapo inazingatia sheria na pale penye shida ya mikataba afike haraka na kuishughulikia pia kufanya ukaguzi katika huduma za afya na usalama mahala pa kazi.

Katika hatua nyingine Mhe. Malima amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imerejesha utaratibu wa kuwapandisha wafanyakazi madaraja, pia kwa mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetoa ajira mbadala 26514 pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia SuluhuHassan ametoa kibali cha kuajiri wafanyakazi 46000 katika kibali hicho ajira za walimu ni 12000 na watumishi wa afya ni nzaidi ya elfu 10000.

Kwa upande wake Mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Morogoro (TUCTA) Nicholaus Ngowi akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa ameiomba Seriksali ifanyie kazi maeneo yote ambayo kunamalalamiko ili kuepusha malalamiko yasio ya lazima kwa Wafanyakazi.

Akibainisha kero za wafanya kazi wa Mkoa wa Morogoro amesema kero kubwa ni mishahara duni ambayo haiendani na gharama za maisha, kuchelewesha nyongeza ya misharaha kwa wanafanyakazi wanaopanda madaraja na marupurupu yao na kutolipwa posho kwa wakati.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.