• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AHIMIZA UPIMAJI AFYA, AMSHUKURU AMIRI JESHI MKUU.

Posted on: August 27th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wanamorogoro kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupima Afya zao na kupatiwa ushauri wa bure na madaktari kutoka taasisi mbalimbali wanaotoa huduma hiyo, ambapo zoezi hilo la upimaji afya linatolewa bila malipo na Jeshi la Ulinzi la  Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Wito huo umetolewa Agosti 27, 2024 na Mkuu huyo wa Mkoa wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo kimkoa yanafanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Morogoro kwa kutoa huduma za Afya kwa wananchi.

Mhe. Malima amesema katika kuadhimisha maazimisho hayo,  Jeshi hilo linatoa huduma za Afya zikiwemo upimaji wa macho, saratani ya shingo ya kizani na matiti kwa wananwake, upimaji wa tezi dume na huduma mbalimbali za kiafya hivyo amewata wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwenda kupima afya zao na kila mmoja anapopata huduma akawe balozi kwa mwenzake ili watu wazidi kujitokeza kwa wingi kupima Afya zao.

"... Naomba nichukue fursa hii niwasihi sisi sote tuliokuwa hapa tutumie nafasi hii twende tukapime Afya zetu, na tukitoka hapa twende tukawe mabalozi kwa wenzetu.."

Aidha Kiongozi huyo amelishukuru Jeshi hilo kwa huduma wanayotoa ya upimaji wa Afya bila malipo kwa wananchi wa Morogoro na isiwe mwisho kutoa huduma hiyo ya Afya bali waendelee kuitoa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali zilizopo mkoani humo.

Katika hatua nyingine Mhe. Adam Malima amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutoa matibabu hayo bila malipo kwa wananchi wa Morogoro pia  kuliongoza jeshi hilo na kuendelea kuwa imara zaidi ambapo imepelekea kujulikana kitaifa na kimataifa.

Sanjari na hayo Mhe.  Malima amewataka Wananchi hasa wakinamama wajenge utamaduni wa kupima afya zao mara hususan magonjwa ya  saratani katika mlango wa kizazi na matiti kwa lengo la kupata tiba mapema ili kukabiliana na changamato ya magonjwa hayo katika  jamii huku akiwataka akinababa kujengea mazoea ya kupima tezi dume ili kuwahi matibabu pindi wanapogundulika kuwa unaugonjwa huo.


Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga na Mkuu wa Kikosi cha Jeshi Mazao Brigedia Jenerali Seif Athumani Hamisi amesema shughuli ya utoaji wa huduma za Afya kwa Mkoa wa Morogoro zimeanza Agosti 26, 2024 na zimelenga kutoa huduma za upimaji bure kwa wananchi ambapo zoezi hilo litadumu ndani ya siku 5, hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupima Afya huku akibainisha huduma inayotolewa ni kwa magonjwa kama macho, saratani ya shingo ya kizazi na matiti, tezi dume, presha, kisukari na mengine mengi.

Naye Bi. Agnes sepeku mkazi wa manispaa ya morogoro akiwa amepata mara baada ya kupata huduma amesema huduma zinazotolewa ni zuri na zinatolewa kwa haraka  ambapo amewataka wanamorogoro kujitokeza kwenda upima afya zao kwani hakuna gharama yoyote.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.