Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili ofisini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakibadilishana mawazo kabla ya hafla ya makabidhiano rasmi ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema Mkoa wa Morogoro una fursa nyingi za kiuchumi ambazo zikitumiwa vizuri uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla utakua.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa (kulia) wakisaini nyaraka za Makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mhe. Malima ametoa kauli hiyo Juni 1 mwaka huu kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Fatma Mwassa katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema pamoja na Mkoa huo kushika nafasi ya kwanza kwenye uzalishaji wa chakula hapa nchini lakini kuna haja ya Mkoa kuweka mikakati bora ili kuhakikisha kuwa Mkoa huo unashika nafasi ya kwanza kwa uzalishaji wa Chakula.
Mhe. Fatma Mwassa (kulia) akikabidhi nyaraka za serikali kwa Mhe. Adam Malima (kushoto) ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi ofisi hiyo.
"...tunaenda kujadiliana pale ambapo tunakuwa mtu wa tano au wa nne, kwa nini tusiwe wa kwanza, kinachotukwaza tusiwe mtu wa kwanza ni nini?..." amesema Mhe. Adam Malima.
Aidha, Mhe. Adam Malima amesema mifugo ya Morogoro lazima iwe na mchango kiuchumi ndani ya Mkoa huo na Taifa kwa jumla ndani vinginevyo kitakuwa hakuna maana.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akizungumza na viongozi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amemuhakikishia Mhe. Fatma Mwassa kuwa ataendeleza mazuri aliyoyaacha katika Mkoa huo pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali.
Awali, Mhe. Fatma Mwassa ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera amemuhakikishia Mhe. Adam Malima kupata ushirikiano kutoka kwake ili kufanikisha harakati za kuwaletea wanamorogoro maendeleo.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera akitoa taarifa fupi ya Mkoa huo kabla ya kukabidhi rasmi ofisi hiyo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo amemshukuru Mhe. Fatma Mwassa kwa uongozi wake uliotukuka katika kuhakikisha kuwa viongozi ndani ya Mkoa huo wanakuwa na maono ya pamoja.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba akitoa neno la shukurani na la ukaribisho kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Picha ya pamoja wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya kiofisi baina ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa MKoa wa Kagera. kutoka kushoto waliokaa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa, Mhe. Adam Kighoma Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Abubakari Mwassa na Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Morogoro Joseph Masunga
Hawa ni baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. wakuu wa Mikoa ya Morogoro na Kagera baada ya makabidhiano ya kiofisi
Waliosimama ni baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kushoto ni Alhaji Hamis Sengulo, katikati ni Ndg. Solomon Kasaba na kulia ni Jamila Miyonga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahe. Wakuu wa Mikoa ya Morogoro na Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (wa pili kushoto waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa dini wa Mkoa wa Morogoro baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (wa pili kushoto waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (wa pili kutoka kushoto waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.