• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima akasirishwa na tabia ya wafugaji kuingiza mifugo hifadhini.

Posted on: January 19th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amekasirishwa na tabia ya wananchi hasa wafugaji wa Mkoani humo wanaoingiza mifugo yao kwenye hifadhi na kusababisha uharibifu wa mazingira.

Mhe Malima ametoa kauli hiyo Januari 18, 2024 wakati wa ziara yake na kutembelea pori la akiba la mto Kilombero lililopo Wilayani Kilombero   ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa huo.

Mhe. Malima amesema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) wanampango wa kutengeneza msitu wa hifadhi unaozunguka hifadhi nzima utakaokuwa na upana wa mita 200  ili kuzuia Wafugaji kutoingiza mifugo yao katika eneo la hifadhi hiyo.

“….Hakuna mtu anauchukia ufugaji, Tunataka ufugaji uwe endelevu ili uwe na manufaa kwa Tanzania kwa miaka 50 ijayo na wakulima wawepo, na ng’ombe ziwepo, hatuishi kwa ajili ya leo tu….” amesema RC Malima.

Pia Mhe. Adama Malima amesema, wana lengo la kuwawekea hereni ng’ombe wote watakaokuwepo eneo la  bonde la Mto Kilombero ili kufahamu idadi yao katika eneo hilo, hivyo kuwa rahisi kujua wanapoongezeka na kuchukua hatua mapema.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa wafugaji wanaolisha mazao ya wananchi kwa makusudi watakaobainika watalipa hasara yote itakayotokea, na kwamba hataki kusikia migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa sababu pande hizo mbili zinategemeana, kwa wafugaji kupata malisho na wakulima kupata mbolea kutoka kwa wafugaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafugaji Kijiji cha Miwangani Parasoi Ndimba amesema wapo tayari kupunguza idadi ya mifugo na kupangiwa maeneo mengine kulingana na idadi ya mifugo wanayomiliki ili kupunguza ongezeko la mifugo katika eneo hilo.

Hata hivyo mwenyekiti huyo amemuomba Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Malima kutatua changamoto ya maji wanayokumbana nayo hususan kipindi cha kiangazi hasa katika Kitongoji cha Miwangani ambapo tatizo hilo kwa sasa limekuwa sugu.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.