• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AKEMEA UKATILI WA KIJINSIA KWA WAJANE

Posted on: June 23rd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amekemea vikali ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa wajane kutokana na kuwepo kwa mila na desturi kandamizi katika jamii na kufanya maisha ya wajane kuwa magumu zaidi baada ya kufiwa na Waume zao.

Mhe. Malima ametoa karipio hilo Juni 23, 2024 wakati wa maadhimisho ya siku ya Wajane duniani katika Viwanja vya Kiwanja cha ndege kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo yakiwa na lengo la kubaini changamoto za wajane na kutafutia ufumbuzi, kusimamia haki na kudumisha upendo baina yao.

"...semeni mtapata msaada wa haraka... na nina maafisa maendeleo kutoka ofisini kwangu ili mjue serikali ni moja na  inahakikisha hamnyanyaswi na ujane..." amesema Mhe. Adam Malima 


Aidha, Mhe. Adam amesisitiza Chama cha wanawake wajane Tanzania - CCWWT kuweka utaratibu wa kutegemea Sheria kwa kushirikiana na mahakama ili kuwa na mifumo wezeshi mfano Dawati la Jinsia katika kupinga ukatili kwa kina mama na kupata haki zao ukiwemo urithi wa mali.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesema chama hicho kina jukumu la kutoa elimu na ushauri wa kisheria kwa wajane Milioni 1.4 kutokana na sensa ya mwaka 2022 hapa nchini ili kujua namna ya kupata haki zao pasipo kutegemea vikao vya mila vinavyodidimiza maslahi ya kina mama wajane kwani Serikali inatambua na kuthamini uwepo wa wajane hao.


Sambamba na hilo, Mhe. Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kutambua umuhimu wa kina mama na kufanya jitihada kuja na mpango wa nishati safi kwa matumizi ya nyumbani kuepuka uharibifu wa mazingira kwa ukataji miti ovyo na kuondoa magonjwa yatokanayo na moshi wa kuni.


Kwa upande wake, Mratibu wa Wajane Taifa ( Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalum) Bi. Bahati MaJwala amesema maadhimisho hayo yanasaidia kuongeza uelewa kwa Jamii kuhusu mila na desturi hivyo kuwajengea uwezo wajane kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Naye, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Bi. Mary Carlos Kallomo amesema mahakama imeboresha mifumo na kuhakikisha inawawezesha watu wote hapa nchini  wakiwemo wznawake wajane kupata haki zao za msingi.

Kwa niaba ya Wanawake wajane, Katibu wa Chama cha Wajane Tanzania Bi. Sabrina Tenganamba amesema kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 idadi ya wanawake wajane imefikia Milioni 1.8 hapa nchini huku akibainisha kuwa ndugu wa wajane hao hawaruhusiwi  kuchukua mali zao bali hurithiwa na watoto pamoja na Mama zao.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.