• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA ARIDHIKA NA UJENZI WA DARAJA LA RUAHA, AMSHUKURU RAIS, WADAU NA WANAHABARI

Posted on: May 3rd, 2024

RC MALIMA ARIDHIKA NA UJENZI WA DARAJA LA RUAHA, AMSHUKURU RAIS, WADAU NA WANAHABARI

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam kighoma Malima ameridhika na maendeleo ya ujenzi wa daraja la mto Ruaha baada ya kufika eneo la ujenzi na kukuta kazi zinaendelea kufanyika huku ikiwa imebaki asilimia 9 tu ujenzi wa Daraja hilo kukamilika.

Hayo yamebainika Mei Mosi, 2024 wakati Mhe. Kighoma malima alipofanya ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake ulisimama kutokana na Mvua zilizokuwa zinanyesha.

Mhe. Malima amesema,  ujenzi wa daraja hilo kwa sasa  unaendelea vizuri baada ya hali ya mvua kusimama na ujenzi kuendelea na kupelekea watu kuvuka kwa miguu kutoka upande mmoja hadi mwingine na kuleta matumaini ya kukamilika kwa Daraja hilo.

“….lakini namshaukuru mwenyezi mungu (at least - angalau) hapa tulipo Daraja kutoka upande mmoja hadi upande mwingine limeezekwa kama sote tulivojionea…” Amesema Mhe. Malima 


Katika hatua nyingine, Mhe. Kighoma Malima ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa maelekezo Mawaziri na Watendaji wengine kufika Mkoani Morogoro na kujionea hali halisi ya mafuriko na kutoa Ushauri na misaada mbalimbali, ombi lake kubwa na kuiomba Serikali kufungua mawasiliano kwa maeneo ambayo bado hayajafunguka.

“…tunachotaka sisi ni kufunguliwa tu mawasiliano…” amesema Adam Malima

Aidha, amewashukuru wadau wote waliojitokeza na wanaoendelea kujitokeza kutoa misaada ya hali na mali kwa wananchi wa Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga waliofikwa na mafuriko yaliyotokana na mvua nyingi zilizonyesha kipindi kifupi kilichopita.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu, amewashukuru waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro kwa kutoa taarifa sahihi kuonesha uhalisia wa mafuriko yaliyotokea ndani ya Mkoa wa Morogoro hususani wilaya za Kilombero, Mlimba na Ulanga na kupelekea viongozi wa kitaifa kufika na kujionea hali ya mafuriko hayo.

Kwa upande wake Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Daraja hilo akiongelea ujenzi wa Daraja la Ruaha amesema ujenzi huo umefikia asilimia 91, na ujenzi wa mradi wote wa Barabara ya Kidatu -  Ifakara kwa jumla umefikia asilimia 89 huku akibainisha kuwa daraja hilo litakamilika katikati ya mwezi Juni, mwaka huu endapo mvua hazita endelea kunyesha.

Wananchi wa Wilaya ya Kilosa na Kilombero wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga Daraja hilo kubwa kwani wamesema awali kulikuwa na changamoto ya watu kugombania kupita kwa vile lilikuwa jembamba, lakini pia Daraja la zamani lilikuwa lina vyuma juu kiasi kwamba kama kuna gari ina mizigo mikubwa ililazimu kupunguza kwanza kabla ya kupita.

Hata hivyo wamesema kwa sasa wanafurahi kwa ujio wa Daraja hilo kwa kuwa ni pana linatoa nafasi ya kupishana magari kwa magari bila bughudha huku watu wakiwa wamewekewa njia yao pembeni mwa Daraja hilo lakini pia Daraja hilo litasaidia kuvusha mazao yao kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.