• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AUNDA KAMATI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA HALMASHAURI.

Posted on: June 22nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akisalimiana na Viongozi wa Wilaya na Chama Cha Mapinduzi - CCM baada ya kuwasili ukumbini kwa ajili ya kuanza kikao.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima meunda kamati  maalum itakayo husika kutoa ushauri kwa Halmashauri za Mkoa huo ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kuhusu makusanyo ya  ndani ili kufikia malengo halisi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akisisitiza jambo kwa Wahe. Madiwani wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

Mhe. Malima ameyasema hayo Juni 20 mwaka huu wakati wa kikao cha Baraza maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kilichohusu kujibu Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG za mwaka 2021/2022.

Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ni miongoni mwa Halmashauri nne kati halmashauri tisa za Mkoa huo ambazo zinachangamoto kubwa katika ukusanyaji wa mapato na matumizi yake, na kwamba anaunda timu  itakayopitia taarifa za mapato ya Halmashauri hizo na kufanya tathmini ya taarifa hizo kisha kutoa ushauri wa namna ya kuboresha.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (katikati) akizungumza na Wahe. Madiwani pamoja na Wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya Morogoro wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

"...yapo mengi ya kusema kwenye Halmashauri yenu, nimeteua tume ya uchumi....kwa hiyo hawa mabwana watapita kwenye halmashauri yenu wajadiliane swali moja hadi jingine haswa hili la makadirio..." amesema Mhe. Adam Malima.

Aidha, amewaagiza Wahe. Madiwani kuwa na timu ya kusimamia miradi ya maendeleo katika Halmashauri yao angalau madiwani watatu kwa kila mradi mmoja, kwa kufanya hivyo amesema kutaongeza chachu ya ubora kwenye miradi husika na kukamilika kwa wakati.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo watakao shindwa kwenda na kasi yake katika utendaji  kazi wao kuachia nafasi hizo kabla yeye hajawachukulia hatua.

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya mipango na uratibu Bw. Anza Ameni Ndosa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo, ameisisitiza Halmashauri hiyo kusimamia miradi ya Afya, elimu na maji kwa kuwashirikisha Wahe. Madiwani ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ubora unaohitajika.

Naye, Mkaguzi wa nje na mdhibiti wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Morogoro CPA Peter Mwabwanga amesema katika  kipindi cha miaka mitatu 2019 hadi 2021 wanafunzi wanne kati ya kumi wa Sekondari wa Halmashauri hiyo waliacha shule, na kuwataka kuweka mikakati mahsusi ya kuhakikisha wanadhibiti suala hilo.

Mkaguzi wa nje na mdhibiti wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Morogoro CPA Peter Mwabwanga akitoa ufafanuzi wa hoja za CAG wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

Baada ya majadiliano ya kina Mkuu wa Mkoa ameagiza kiwepo kikao kingine cha baraza la madiwani ambacho kitafanyika mwezi Julai mwaka huu huku akiwataka wajumbe wa menejimenti ya Halmashauri hiyo  kuja na hoja na majibu yanayojitosheleza.

Baadhi ya Wahe. Madiwani wakiwa kwenye kikao.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.