Mkuu waMkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amefanya kikao na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali, chama, Wakuu wa taasisi za umma na binafsi na wafanyabiashara kwa lengo la kujadiliana njia sahihi ya kuyafikia mafanikio tarajiwa ya Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro.
Kikao hicho kimefanyika Juni 1 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo wadau mbalimbali wa maendeleo wamehudhuria.
Mhe. Malima amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kujadiliana kwa pamoja ili kuwa na muelekeo mmoja wa kuyafikia mafanikio ya Mkoa huo.
"...tuzungumze na wadau wote tufahamiane na tuelewane katika hili tunalotaka kulifanya na nini tunatarajia kufanya kwa ajili ya mafanikio mapana ya Mko wetu..." amesema Mkuu wa Mkoa.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye kikao cha kujadili muelekeo wa Mkoa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amezisisitiza taasisi za umma Mkoani humo kuwa na mahusiano mazuri ili kufanikisha utendaji kazi wa taasisi hizo, akitolea mfano Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatakiwa kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara kwa kuwa ndio wanao changia pato la Mkoa kupitia ushuru na kodi wanazozitoa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (aliyevaa kofia) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama Mkoa wa Morogoro Bw. Aloyce Mbena baada ya kikao cha kujadili muelekeo wa Mkoa huo.
Nao wao wakuu wa taasisi mbalimbali walipata nafasi ya kuchangia hoja kwenye kikao hicho akiwemo Mtendaji Mkuu wa Chemba ya kilimo, biashara na viwanda Tanzania (TCCIA)Bw. Moumin Mwatawala amesema Serikali kupitia Wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) pamoja na (TANROADs) kurekebisha barabara zilizopo kwenye maeneo yanayo kusanya wafanyabiashara mbalimbali kama vile maeneo ya sokoni, standi na viwandani kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na malighafi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kusirye Ukio akielezea hali ya huduma za afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wake Meneja wa sheria na utawala kiwanda cha nguo cha 21st Century Bw. Nikodemus Mwaipungu amesema uzalishaji wa kiwanda hicho umepungua kutokana na changamoto ya kukatika kwa umeme na maji hivyo ameomba mamlaka husika kulifanyia kazi suala hilo ili kuongeza uzalishaji.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye kikao cha kujadili muelekeo wa Mkoa wa Morogoro.
Nae Bi. Esther Mwigude ambaye ni msimamizi wa kiwanja cha ndege Morogoro kwa niaba ya Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) ameeleza mikakati ya uanzishawaji wa kiwanda kidogo cha kuunganisha vipuli vya ndege za abiria wawili, pamoja na kufungua chuo cha mafunzo ya rubani katika kiwanja cha ndege kilichopo katika Manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa (wa pili kutoka kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Morogoro Ndg. Fikiri Juma wakiwa kwenye kikao.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kihanga akichangia hoja kwenye kikao cha majadiliano ya muelekeo wa Mkoa wa Morogoro.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.