• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Morogoro ataka msitu wa Kuni Ulindwe

Posted on: September 15th, 2022

RC Morogoro apiga ‘stop’ wananchi kuvamia Msitu wa Kuni, Atoa somo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amepiga marufuku kwa mwananchi yeyote kuendelea kufanya shughuli za Kibinadamu ndani ya msitu wa Hifadhi unaojulikana kama  msitu wa Kuni uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa upande Mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria za uhifadhi.

RC Fatma Mwassa (Mbele) akiongea na baadhi ya wananchi wanaosadikika kuwa wamevamia Hifadhi ya msitu wa Kuni

Fatma Mwassa ametoa agizo hilo Septemba 15, 2022 baada ya kuanza ziara yake ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa lengo la kujitambulisha, kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi ndani ya Wilaya ya Mvomero.

Amesema, msitu huo uko kisheria, hata hivyo kuna watu wanaendelea kuuvamia msitu huo na kujenga nyumba bila vibali halali, hali ambayo ni hatari kwao kwa kuwa wanafanya kosa na ni uhalifu kama uhalifu mwingine hivyo kuwataka wananchi hao wasiuze wala kununua eneo lolote ndani yam situ huo kwani wanatapeliwa.

“narudia tena kuwaambia, usinunue Ardhi wala kwa mtendaji wa Kijiji, wala kwa Mtendaji wa Mtaa wala kwa Mwenyekiti wa kijiji, hiyo Ardhi sio mali yao wao, mnapofanya hivyo mnatapeliwa” amesema Fatma Mwassa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ametoa uelewa kwa wananchi waliofika eneo la msitu wa kuni kwa kuwaeleza utaratibu wa kupata kiwanja kwa kuzingatia sheria, taratibu na Kanuni na miongozo inayohusu Ardhi na si vinginevyo.

Akibainisha hilo Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa amesema ili kujenga nyumba ni lazima mwananchi awe ametekeleza mambo muhimu mawili: kuwa na hati miliki ya Ardhi na pili kuwa kupata kibali cha ujenzi wa nyumba anayotaka kujenga na vyote hivyo vinapatikana Ofisi za Ardhi za Halmashauri husika na sio kwa Mtendaji wa Kijiji wala Mtaa.

wananchi wa Eneo la msitu wa kuni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alipofika eneo la hifadhi kujionea namna lilivyovamiwa na wananchi

Aidha amemuagiza Afisa Mhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania {TFS} kuhakikisha wanalinda msitu huo na kuweka matangazo ya katazo la kujenga ndani yam situ huo na kuchora alama  X au kuandika maneno ‘BOMOA’ kwenye majengo yote yaliyojengwa ndani ya msitu huo, huku akiwataka wananchi waliokwisha anza kuishi ndani ya Msitu wa kuni kutofanya chochote hadi pale watakapoambiwa vingine na Serikali.

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.