• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MOROGORO AWAAGIZA TANROADS NA TARURA

Posted on: March 6th, 2023

Mhe. Fatma Mwassa  Akifungua kikao cha Bodi ya Barabara leo tarehe 6 Mwezi wa Tatu Ukumbi wa Hoteli ya Morena 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amewaagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Vijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro kuwachukulia hatua za mapema wale wote wanaojenga au kufanya shughuli zao kwenye hifadhi za barabara ili kuepuka usumbufu wa kubomolewa wakati nyumba au majengo yao yakiwa yamekamilika.

Meneja wa Bodi ya Barabara (Eng Alinanuswe Kyamba) Akitoa Tarifa ya utekelezaji wa Miundombinu ya Barabara Mkoani Morogoro

Mhe. Fatma Mwassa ametoa agizo hilo Machi 6 mwaka huu wakati akifungua kikao cha Bodi ya barabara cha Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Morena iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Mhe. Fatma Mwassa amewaagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Vijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro leo. 

Amesema, hakuna mantiki kuwaacha wananchi wakiendelea na ujenzi kwenye hifadhi za barabara hadi wanakamilisha ujenzi na kisha kuja kuwabomolea wakiwa wamekamilisha, ni vema kuwachukulia hatua mapema kwa kusitisha ujenzi wakiwa katika hatua za msingi na kisha kutoa Elimu ya kutojenga maeneo hayo ili kuepuka usumbufu wa kubomolewa majengo yao.

“...kwenye hili niwaombe sana TARURA na TANROADS mtu anapoanza tu kujenga anatakiwa kubomolewe pale pale ...ananza tu kuchimba msingi mnabomoa na kumuelimishwa kwamba hapa hapaswi kujenga...” amesema Mhe. Fatma Mwassa.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara zikiwemo alama za barabarani, vivuko, na kingo za madaraja ya chuma ambapo hadi sasa takribani alama 19 zimeibiwa kwenye barabara mpya ya Ludewa – Kilosa Wilayani.

 Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Leo ukumbi wa Morena


Mkuu huyo wa Mkoa amesema niwajibu wa kila mwananchi kulinda, kutunza miundo mbinu ya barabara, vivuko na alama za barabarani zinazowekwa ili alama hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu.

“...naagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa yeyote atakaebainika kuhujumu miundombinu ya barabara zetu au kwa uharibifu wa aina yoyote ile...” amesema Mhe. Fatma Mwassa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Meneja wa TANROADS na TARURA kuwatumia wakandarasi wa ndani ya MKoa (wazawa) wenye sifa za kutengeneza barabara ili kukuza uchumi wa Mkoa huo.

Hata hivyo ametoa rai kwa Wakandarasi wote wanaopewa kazi za ujenzi wa miundombinu katika Mkoa huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi na kukamilisha kazi zao kwa mujibu wa mikataba waliyosaini.

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mussa Ali Mussa

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.