• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC SHIGELA AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MALINYI, AZINDUA UJENZI WA JENGO LA DHARURA

Posted on: March 6th, 2022

RC Shigela azindua ujenzi wa jengo la Dharura Malinyi, asema hana mgogoro nao, ataka viongozi kushikamana.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigella amezindua ujenzi wa jengo la dharura litakaloghalimu shilingi milioni 390 katika hospitali ya wilaya ya Malinyi ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa majengo ya hospitali hiyo huku akipongeza mabadiliko ya kiutendaji yaliyopo sasa na kutaka waendelee kushikamana.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akikagua ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Malinyi Machi 5 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni akiwa Wilayani humo katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo yanayojengwa baada ya kupokea fedha shilingi milioni 500 kkutoka kwa Serikalini na milioni 390 kwa ajili ya jengo la Dharura ambalo ujenzi wake umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa siku alipotembelea.

Akiwa katika eneo hilo Martine Shigela alikagua ujenzi wa jengo la mionzi, maabara, jengo la kufulia nguo, utawala, jengo la kutolea dawa pamoja na majengo mengine na kuridhika na meandeleo ya ujenzi unavyoendelea na kumpongeza Mkuu wa wilaya Mathayo Masele pamoja na Mkurugenzi Joanfaith Kataraia kwa niaba ya viongozi wengine kwa kusimamia vyema ujenzi huo.

Amesema, kwa sasa hana mgogoro na Viongozi wa Wilaya hiyo kwa kuwa wanafanya kazi kwa weledi, Mshikamano, ushirikiano na umoja huku akiwataka kuendeleza hayo na hasa kusikiliza kero za wananchi waliopo katika Wilaya yao.

“kwa hiyo nataka niwasihi tena sina mgogoro na Malinyi sasa, mkiona nimekuja hapa kueni na Amani chapeni kaz, mkiona kiongozi mkubwa amekuja mimi nitawasemea vizuri mimi Mkuu wa MKoa” amesisitiza Martine Shigela.

Akimkaribisha kuzungumza na wananchi waliojitokeza katika eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya hiyo Mathayo Masele amesema pamoja na changamoto chache ambazo bado zipo, changamoto hizo hazitawazuia kuwatumikia wananchi kwa kuwa hizo hazitakuwa dawa ya malaria au kero nyingine walizonazo wananchi wa Malinyi huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Joanfaith Kataraia pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwapelekea shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi Hospitali na milioni 390 jengo la dharura,ameahidi mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa Halmashauri hiyo kamwe haitokuwa tena na historia ya kutomaliza miradi ya maendeleo.


Kwa upande wao wananchi wa Malinyi Asha msenga na Eleonara Mlombole wamempongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya ambayo imeondoa kero walizokuwa wanazipata kutoka Hospitali za Binafsi ikiwemo kubaki Hospitalini endapo  hujamaliza kulipa  deni la matibabu hata kama umepona suala ambalo kwao lilikuwa kero kwao.


Pamoja na shukrani hizo wamemuomba Mhe. Samia Suluhu Hassan kukamilisha majengo ambayo hayajakamilika yakiwemo nyumba ya kujifungulia waja wazito, Mochwari, jengo la dharura na jengo la kulala wanaotunza wagonjwa kwani kutokuwepo majengo hayo kunapelekea adha kwao.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.