• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Serikali yamwaga zaidi ya Tsh bil 26 za barabara Mkoani Morogoro, Mkuu wa Mkoa Adam Malima ashuhudia utoaji Saini.

Posted on: September 13th, 2023

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi Bil. 26.3 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya Barabara za Mkoa wa Morogoro huku Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Kighoma Malima akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa barabara hizo na kubainisha kuwa serikali imedhamilia kuleta mageuzi ya maendeleo kwenye maeneo ambayo hayafikiki kirahisi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikata utepe mikataba ya Barabara akishikiwa na Meneja wa TARURA Bw. Emmanuel Ndyamukama.

Rc Malima akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya Barabara.

Mhe. Adam Malima amebainisha hayo Septemba 12, 2023 wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya barabara kati ya Wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) na Wakandarasi, yenye thamani ya shilingi Bil. 26,377,060,200.00 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima (hayupo pichani).

Amesema, wananchi wanatakiwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita wa kuwafikia watanzania wengi kwani mikataba kama hiyo inalenga kuwaletea maendeleo yao kupitia ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya barabara, huku akiwataka wakandarasi waliosaini mikataba kukamilisha miradi yao kwa muda uliopangwa ili kuepuka ongezeko la gharama kwa miradi waliyoisaini.

"... lazima tufike sehemu tutambue mchango wa Serikali unaofanywa katika kuifikia jamii na watanzania na haya ndio maendeleo tunayotakiwa tuyafikie tukiyasimamia, nasema haya kwa sababu tuna mradi wa barabara wa Tsh Bilioni 26.3 nimewaambia miradi inatime framing tukikaa na mradi kwa miezi 8 hadi miezi 18 hujamaliza ni disaster..." amesema Mhe Adam Malima.

Katika hatua nyingine, Mhe. Malima amewataka viongozi wa Mamlaka ya mapato Tanzania - TRA kutoa mapema vifaa vya ujenzi vinavyopita bandarini ili kuondoa changamoto hiyo ambayo imekuwa ni kisingizio kwa baadhi yao cha kutokamilisha  miradi yao huku Afisa usimamizi wa Kodi idara ya elimu na mawasiliano wa Mkoa huo Bw. Lutufyo Mtafya  akiahidi kulifanyia kazi agizo hilo.

Sambamba na hilo, Mhe. Malima amesema  utekelezaji wa miradi hiyo unahitaji umoja na ushirikishwaji hivyo amewaomba wahe. Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Madiwani, viongozi wengine na wananchi kwa jumla, kushirikiana na kuona kuwa miradi hiyo siyo ya Serikali ni miradi  yao hivyo kuisimamia na kuilinda.

Kwa sababu hiyo, amewataka Wakandarasi hao waliotia saini mikataba hiyo watakapokifika kwenye maeneo yao wawashirikishe wadau wote muhimu katika utekelezaji wa miradi hiyo na hivyo kuwafanya kuwa ni miradi yao (ownership).

Awali, Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro Bw. Emmanuel Ndyamukama amesema fedha hizo Bil.26.3 zimelenga kufanyia matengenezo mbalimbali ya barabara, fedha ambazo zitatoka katika mfuko wa barabara Tsh. bilioni 8.6, fedha za tozo Tsh. Bil. 12.2 na fedha za mfuko wa Jimbo Tsh. Bil. 5.5 na kuleta jumla ya Tsh. 26.3 ambapo fedha hizo zitakazotumika kutengeneza barabara na kuunganisha maeneo yote yenye shughuli za kiuchumi kama kilimo, Utalii na madini.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro Bw. Emmanuel Ndyamukama akitoa taarifa kuhusu mikataba hiyo ya barabara.


Nae Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge  wote Mkoa wa Morogoro, kwa niaba yao, amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha Sh. Bil. 26.3 Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuwahudumia wananchi kwenye sekta hiyo ya miundombinu.


Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge  wa Mkoa wa Morogoro akitoa salamu za Wabunge wa Mkoa huo katika hafla hiyo.

Aidha, ametaka Wakandarasi waliopewa tenda ya ujenzi wa barabara mkoani humo, kutekeleza miradi hiyo kwa ubora unaotakiwa huku akiwataka kubadilika na kufanya kazi zao kwa umahili  ili tenda hizo waendelee kupewa wao kama wazawa badala ya wageni.

Amesema, ni jambo la kusikitisha wakandarasi wa kitanzania wakipewa kazi na wakandarasi wageni kufanya kazi kama wahandisi wanafanya kazi nzuri sana, lakini wakiaminiwa na kupewa kazi hizo kama wakandarasi hawafanyi vizuri na kuwataka wabadilike ili kazi nyingi za ukandarasi hapa nchini wapewe watanzania wenyewe.

TARURA itaingia Mikataba na Wakandarasi 82 yenye thamani ya jumla ya zaidi ya Tsh. Bil. 26.3 ambapo leo imesainiwa mikataba 23 yenye thamani ya shilingi Bil. 6.13 huku mikakati ya TARURA Mkoa wa Morogoro ili kufikia malengo wamedhamiria kudhibiti muda wa utekelezaji miradi, kudhibiti gharama, kudhibiti ujenzi wa viwango na kuhakikisha wadau wote muhim wanashirikishwa.

MWISHO.


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.