• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Serikali yapiga marufuku matumizi ya kamba za plastiki

Posted on: September 14th, 2021

Serikali nchini imepiga marufuku matumizi ya kamba za plastiki  kwa taasisi zote za Serikali na kuagiza kutumika kwa kamba zinazotokana na  zao la  Mkonge ili kuongeza soko la uhakika kwa wakulima wa Mkonge.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa Mkutano wa pili wa wadau wa sekta ya Mkonge uliofanyika Septemba 13 mwaka huu Ilonga Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Bashe akiangalia bidhaa zinazotengenezwa kutokana na zao la Mkonge.

Mhe. Bashe amesema sio tu matumizi ya kamba za Plastiki zinachangia kwa asilimia kubwa kupunguza soko la Mkonge lakini pia mifuko hiyo inauzwa pasina kuwa na nembo ya ubora na zinazalishwa na viwanda bubu ambavyo havijasajiriwa na Serikali.

‘’…Naiagiza Wizara ya Kilimo kutoa tamko la kisera kuzuia matumizi ya kamba za plastiki katika kufungashia mazao mbalimbali na taasisi zote za Serikali  ni marufuku kutumia kamba za plastiki badala yake watumia kamba za katani ….’’ amesema Bashe.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela (wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa huo kabla ya kuwasili mgeni rasmi katika Mkutano huo

Naibu Waziri Bashe amemwagiza Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania - TARI na Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania kuhakikisha wanakuwa na Ofisi ndogo ya zao la Mkonge Wilayani Kilosa na kuazisha kitalu cha uzalishaji miche kwa ajili ya wakulima wa zao hilo waliopo Mkoani  Morogoro.

Katika hatua nyingine, Waziri Bashe ameitaka TARI kuwasaidia wakulima wadogo kutumia mbinu  bora za  kilimo ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu kwa wakulima kumudu utunzaji wa mashamba na kuwapatia mafunzo ya ugani ynayolenga kutumia eneo dogo la shamba litakalotoa mavuno mengi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amesema Mkoa wa Morogoro umejipanga vizuri kuwasaidia wakulima wa zao la Mkonge kuhakikisha wanafanya block farming, kuainisha mashamba ya Mkonge na kushirikiana na TARI katika kuwasaidia wakulima kuwapa mashine za kusindika zao hilo la  Mkonge.

Sambamba na hayo, amewataka wadau na taasisi za fedha na mifuko ya kijamii Mkoani humo ikiwemo NSSF kujipanga kuleta mashine za kusindika Mkonge ili wakulima wasitumie mashine ndogo  zilizopo sasa ambazo haziwezi kutoa Mkonge wenye ubora unaohitajika.

Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro Denis Londo akieleza suala nzima la zao la Mkonge.

Aidha, Shigela amewatoa hofu wakulima wa zao hilo kuwa watahakikisha wanawathibiti wafugaji wanaolishia mifugo mazao yaliyopo kwenye mashamba yao na kuwaahidi kutatua changamoto ya Tembo wanaovamia mazao ya wakulima.

Wakizungumzia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika zao la Mkonge akiwemo Mwenyekiti wa wadau wa zao la  Mkonge Damian Luhinda amebainisha changamoto anazokumbana nazo kwenye kilimo hicho kuwa ni ukosefu wa mitaji, ushindani wa bidhaa za Plastiki na kuongezeka kwa kodi.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Mkonge Bi. Mariam Nkumbi ameiomba Serikali kuthibiti changamoto ya Tembo wanaovamia mashamba ya wakulima wakiwemo wakulima wa zao la Mkonge ambao kusababisha hasara kubwa kwao jambo linalopelekea wakulima hao kukata tamaa ya kuendelea kulima zao hilo.

Mkutanao wa kwanza  wa Wadau wa uhamasishaji wa zao hilo la Mkonge  ulifanyika mjini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, huku mkutano wa sasa uliofanyika hapa Kilosa ni mkutano wa pili ambapo Waziri Mkuu amewakilishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

 

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.