Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amesema Katibu Tawala wa Mkoa huo anayemaliza muda wake wa Utumishi Serikalini Bi. Mariam Mtunguja alikuwa ana uwezo Mkubwa wa kuongoza watumishi walio chini yake na kufanya kazi kwa ushirikiano hali iliyopelekea Mkoa huo kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri zake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akieleza uwezo alionesha Bi. Mariam Mtunguja wakati akiwa kazini jana kwenye hafla ya kumuaga na wastaafu wenzake Julai 15 Mwaka huu.
Martine Shigela amesema hayo Julai 15 2022, wakati wa hafla ya kumuaga Bi. Mariama Mtunguja na watumishi wengine 12 wa Sekretarieti ya Mkoa huo ambao wamestaafu utumishi wao Serikalini hafla iliyofanyika katika viwanja vya Makazi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Majid Mwanga akimkabidhi zawadi Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Ezron Kilamhama akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo kutoa neno kwa Katibu Tawala Mstaafu Bi. Mariam Mtunguja.
Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Utawala na Utumishi Herman Tesha akionekana kumkabidhi zawadi Bi. Mariam Mtunguja wakati wa hafla ya kumuaga
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa ambao utumishi umekoma hivi karibuni wakiwa tayari kushuhudia keki ikikatwa kwa ajili yao
Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa amesema Mariam Mtunguja alikuwa ana utamaduni wa kufanya kazi kwa kupenda kushirikisha na kutaka watumishi kufanya kazi kwa pamoja (team work) jambo ambalo anasema lilibadilisha utendaji wa kazi wa watumishi wa Mkoa huo na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Akifafanua zaidi Mkuu huyo wa Mkoa amesema wakati Katibu Tawala huyo anashika uongozi wa Mkoa huo mwishoni mwaka wa fedha (2020/2021), Serikali ilikuwa imeupangia Mkoa huo kukusanya fedha kupitia mapato ya ndani shilingi Bilioni 33, na hadi mwaka huo wa fedha unaishi Mkoa ulikuwa umekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 29 sawa na asilimia 88.
Katibu Tawala mstaafu Bi Mariam Mtunguja akikata keki
Furaha na uchungu, Bi Mariamu akikumbatiana na Katibu Muhtasi wake ishara ya kuagana
Zawadi pia zilitolewa kwa muagwa, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya (kushoto waliosimama) na timu yake wakimpa zawadi muagwa.
Hii ni timu ya wakilishi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wakitoa zawadi kwa mama
Aidha, Martine Shigela akiakiwahakikishia umati uliokuwepo juu ya uwezo wa Katibu Tawala huyo amesema Kipindi cha mwaka mmoja wa fedha ambacho Bi. Mariamu alikuwepo kwa mwaka mzima (2021/2022) serikali ilipandisha kiwango cha makusanyo ya ndani kwa Mkoa huo kutokashilingi bilioni 33 hadi shilingi bilioni 36, na hadi Juni 30 mwaka huu Mkoa ulikuwa umekusanya shilingi Bilioni 36.1 sawa na asilimia 98, jambo ambalo amesema mafanikio hayo yametokana na mbinu mbalimbali za Katibu Tawala huyo Mstaafu kwa kuwashirikisha watumishi wake kile alicho nacho na kupokea ushauri wao wakiwemo Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri huku akisistiza muda wote kufanya kazi kama timu.
Bi Mariam Mtunguja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro na wa Wilaya
Kwa sababu hiyo Mkuu huyo wa Mkoa amemuahidi Katibu Tawala huyo kuendeleza yote mazuri aliyoyafanya akiwa Mkoani hapo ikiwa ni pamoja na kudumisha utamaduni mzuri aliouazisha wa kufanya kazi kwa ushirikiano.
“Nataka nikuhakikishie Katibu Tawala mstaafu, msingi wa mshikamano uliouacha lazima tuendeleze kwa lengo la kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika Mkoa wetu” amesema Shigela.
kwa upandea wake Bi. Mariam Mtunguja Kwa niaba ya wastaafu wenzake, amesisitiza kudumisha umoja baina ya watumishi wao kwa wao na watumishi na viongozi wao ili kuleta ufanisi mzuri katika kutekeleza majukumu yao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro anayemaliza muda wake wa utumishi Bi. Mariam Mtunguja akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga yeye na wastaafu wenzake, hafla iliyofanyika katika makazi ya Mkuu wa Mkoa huo.
“Niwasihi kuendeleza upendo, umoja na mshikamano baina yenu katika kuupaisha Mkoa wetu wa Morogoro kimaendeleo, Ninyi mnaobaki iwe ndio dira sasa ya utumishi wa mfano” amesisitiza Bi. Mtunguja.
Naye Bi. Hellen Magatti ambaye ni mfanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kwa niaba ya wafanyakazi wenzake ameeleza kuwa Bi. Mariam Mtunguja hakuwa Katibu Tawala tu bali alikuwa Mama na mlezi wa wafanyakazi Mkoani humo kwani aliweza kusikiliza na kutatua changamoto ya kila mfanyakazi ya kikazi na binafsi.
Hellen Magatti mmoja wa watumishi kutoka Sekretarieti ya Mkoa akitoa shukrani za watumishi wa Sekretarieti hiyo ya Mkoa
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.