• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

SHIGELA AMALIZA SINTOFAHAMU WAKULIMA, KIWANDA CHA SUKARI

Posted on: April 28th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ameongoza makubaliano baina ya Wakulima wa miwa katika bonde la Kilombero na Kiwanda cha Sukari cha Kilombero yenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza baina ya pande hizo mbili.

Akizungumza hivi karibuni mara baada ya Kikao cha majumuisho kilichodumu kwa zaidi ya masaa 10 kati ya Uongozi wa Kiwanda hicho na Viongozi wa vyama vya wakulima wa miwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na Kilosa, Shigela amesema yapo makubaliano mengi yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili ambazo zinatarajiwa kuleta tija kwa wakulima pasipo kuathiri uendeshaji wa Kiwanda.

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kila Mkulima kuwa na namba yake binafsi ya utambulisho itakayomwezesha apate malipo stahiki kulingana na kiasi cha miwa alichozalisha badala ya namba ya Mkulima mmoja kutumika na mkulima zaidi ya mmoja.

“Katika kilimo cha miwa ambacho Mkoa wetu ndio kinara, zipo changamoto zilizokuwa zikiwakabili wakulima wetu ikiwemo  baadhi ya wakulima kutokuwa na namba ya utambulisho, tumekubaliana kwamba kila Mkulima atauza miwa kwa kutumia namba yake ya utambulisho na pesa italipwa katika akaunti yake mwenyewe”

Aidha Shigela amebainisha kuwa jambo lingine lililoafikiwa baina ya pande hizo mbili ni kuwepo uwakilishi wa wakulima katika kupima kiwango cha thamani ya sukari iliyotokana na miwa ya Mkulima badala ya kiwango hicho kufahamika baada ya malipo.

Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa amesema Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na Wakulima wa Miwa wameafikiana kwamba Mkandarasi atakayetupa miwa kutokana na kuzidisha uzito wa mzigo wa miwa kwenye gari lake huku akifahamu uzito unaohitajika kuingia kiwandani atawajibika kulipa miwa hiyo kwa pesa zake binafsi.

Shigela amewataka Wakandarasi wanaohusika kubeba miwa ya Wakulima kutoka shambani kuhakikisha wanabeba kulingana na uwezo wa magari yao na kuzingatia kiwango cha uzito kinachohitajika  Kiwandani.

Hata hivyo Shigela amewahakikishia Wakulima wa miwa kwamba Serikali itashughulikia changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za Kilimo cha miwa ikiwemo masuala ya Pembejeo huku akiupongeza Uongozi wa Kiwanda hicho, Viongozi wa Vyama vya Wakulima wa miwa Pamoja na Wakulima wa zao hilo kwa kukubali kukaa Pamoja na kumaliza changamoto zilizojitokeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya mahusiano wa Kiwanda hicho Efraim Mafuru amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa na wakulima wote wa miwa kwamba watayatekeleza makubaliano yote yaliyofikiwa ili kufanikisha ukuaji na uzalishaji wa Kiwanda hicho.

Naye Mwenyekiti wa vyama vya Wakulima wa miwa Bakari Mkangamo amemshuru Mkuu wa Mkoa na  Serikali kwa jumla kwa kufika na kusikiliza changamoto zilizojitokeza na kutumia muda wake wa siku tatu kutatua kero hizo na kuahidi kuongeza uzalishaji wa miwa kupitia wakulima waliopo.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.