• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

SHIGELA APIGA MARUFUKU WAFUGAJI KUINGIZA MIFUGO MASHAMBA YA WAKULIMA, AGOMEA KUWALIPA FAINI.

Posted on: June 13th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amepiga marufuku wafugaji mkoani humo kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu mazao huku akiahdi kukomesha tabia ya wafugaji kulisha mashamba  ya wakulima na kulipa faini kwani amesema tabia hiyo inaendeleza migogoro katika Mkoa huo.


Martine Shigela ametoa maelekezo hayo Juni 12 mwaka huu alipotembelea skimu ya umwagiliaji ya Itete iliyoko Wilayani Malinyi ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake Wilayani humo inayolenga kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.


Shigela amesema baadhi ya wafugaji wamekuwa wakiamini kuwa wana fedha za kulipa faini, pale mifugo yao itakapokamatwa, kwa sababu hiyo hawachukui hatua za makusudi kuzuia mifugo yao kuingia kwenye mashamba ya wakulima wakitegemea kutoa fedha zao kwenye kesi hizo, kwa sababu hiyo Shigela ameelekeza kesi hizo zifikishwe mahakamani badala ya kulipa faini nje ya mahakama.

“Kwa hiyo nielekeze wale wafugaji watakaokuja kulisha na wakakiri kosa wakamlipa mkulima, mwenyekiti wa Kitongoji au mtaa, hizo pesa zipokeeni lakini andikeni barua mpelekeeni Mkuu wa Wilaya. hicho ndicho kitakuwa kielelezo cha kwamba huyo mfugaji aliingiza mifugo, tutampeleka mahakamani kama sehemu ya jinai ya kuhatarisha Amani kwenye eneo husika” ameagiza Shigela.

Wananchi wa Wilaya ya Malinyi hususan wa Skimu hiyo ya umwagiliaji mara nyingi wamekuwa wakilalamikia kero ya mifugo eneo ambalo Disemba 27, 2021 yalitokea mauaji ya mkulima mmoja yaliyosababishwa na migogoro ya pande hizo mbili za wakulima na wafugaji.


mwenyekiti wa jukwaa la mchele Wilaya ya Malinyi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wakulima  Mtimbira Bw. Ekusi Gabriel Ngapulila pamoja na kumshukuru Rais Samia suluhu Hassani kwa kuunga mkono jitihada za wakulima kwa kuwapatia Skimu ya Itete  ametaja changamoto katika kilimo hicho cha umwagiliaji kuwa ni mifugo kuharibu mazao yao husuan mpunga  jambo ambalo linapelekea kukata tamaa ya kilimo hicho.

Mwenyekiti huyo kwa naiaba ya wakulima wenzake ameiomba serikali kuweka mkakati kabambe wa kuhakikisha mifugo haiingii kwenye mashamba yao au kuwatengea wafugaji maeneo yao na kuomba  kuchukua hatua za makusudi na za haraka pale wanapotoa taarifa ya uvamizi wa wafugaji kurisha mashamba yao.


Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Massele amebainisha kuwa Skimu hiyo ina gharama ya shilingi 6.092 Bil. Kwa ajili ya kulima hekta 8,000 lakini hadi sasa zinazolimwa ni hekta 1,000 pekee.

 Aidha, amebainisha kuwa sababu kubwa ya mifugo kuja katika skimu hiyo ni ukosefu wa maji kwa hao mifugo hivyo amesema wanaendelea kutafuta majawabu ya kudumu kwa ajili ya mifugo hao ili wasiweze kufika katika skimu hiyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo ametembelea mradi wa kituo cha Afya cha Itete kilichopewa fedha kiasi cha shilingi 250 Mil. na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 93.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Joanfaith Kataraia kuwaachia wananchi wanaokizunguka Kituo hicho cha Afya ardhi ekari 20 kati ya 35 zilizopo sasa na kuwalipa fidia wananchi wenye ekari 15 zinazotumika kujenga majengo yake ili kuondoa kero na migogoro baina yao na wananchi na Serikali inayoweza kujitokeza siku za  baade kwa kuwa eneo la ekari 15 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya kwa vijijini ni eneo toshelevu.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.