• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

TAIFA GAS YAUNGA MKONO MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Posted on: June 5th, 2024


Hivi karibuni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelekezo kwa Taasisi zote  hapa nchini zinazohudumia chakula watu zaidi ya 100 kusitisha matumizi ya kuni za kupikia chakula, badala yake alielekeza taasisi hizo kuanza kutumia Nishati Safi ya Kupikia, lengo likiwa ni kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kupata kuni na hivyo kusababisha mabadiliko ya tabia nchi.

Kutokana na agizo hilo la Serikali, Kampuni ya Taifa Gas imeamua kuunga mkono agizo hilo la Serikali kwa asilimia mia moja na kuanza mara moja utekelezaji kwa kutembelea Taasisi mbalimbali hapa nchini ili kuhamasisha na kujitangaza ili taasisi hizo ziweze kutumia bidhaa yao ya Taifa Gas.

Leo hii Taifa Gas wapo hapa Mkoani Morogoro katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo wametembelea Taasisi mbalimbali kuona kama taasisi hizo zimeanza kutekeleza agizo la Serikali na kama wanahitaji huduma yao.

Mengi zaidi ungana na Meneja Mauzo wa Taifa Gas Bw. Moses Masawe  ambaye  anaeleza kwa kina lengo la wao kuwepo hapa Morogoro lakini pia anabainisha athari zitokanazo na matumizi ya kuni na mwisho anatoa wito kwa jamii katika kutekeleza agizo la Serikali na namna walivyojipanga kuwahudumia wananchi katika kuwapatia Nishati ya Gesi Safi.

Baadhi ya taasisi zilizotembelewa katika zoezi hilo ni Pamoja na Morogoro Hoteli, Morogoro Sekondari, Shule ya Msingi Mlimani na shule ya Msingi Bungo. Taasisi nyingine ni shule ya Msingi Mchikichini A na  Mchikichini B, pamona  Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo stadi - VETA cha hapa Mkoani Morogoro

Pamoja na changamoto chache zilizojitokeza, kimsingi Taasisi zote zilizotembelewa  leo wanakubaliana na uamuzi huo wa Serikali na wako tayari kutekeleza agizo hilo.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.