• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

UZEMBE WA DEREVA WAGHARIMU MAISHA YA WATU 15.

Posted on: December 18th, 2024



Kamishna wa Operation na Mafunzo Jeshi la Polisi Tanzania CP, Awadhi Juma amesema uzembe wa dereva wa gari la mizigo kwa  kutofuata sheria na kanuni za barabarani ndio chanzo cha ajali iliyopelekea vifo vya watu 15  na kujeruhi watu 7 katika eneo la Mikese barabara ya Morogoro - Dar es Salaam.

CP. Awadhi Juma amebainisha hayo Disemba 18, 2024  wakati akiwa eneo la tukio la  ajali iliyotokea Disemba 17, 2024  iliyohusisha gari la mizigo  na gari ya abiria kugongana uso kwa uso majira ya saa 2 usiku Kata ya Mikese Mkoani Morogoro.

Kamishna wa polisi amesema dereva wa gari hilo hakufuata sheria, taratibu na kanuni za barabarani kwa kujaribu kuyapita magari mengine bila  kujali watumiaji wengine wa barabara.

".. chanzo cha ajali hii inaonyesha kwamba ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alikuwa anatokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro kwa kutaka kuyapita magari ya mbele yake bila kuwa na tahadhari yoyote" amesema CP Awadhi.

Aidha CP. Awadhi amesema  Jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua Madereva  wazembe wanaosababisha ajali barabarani na kutoa wito kwa madereva wote nchini kuzingatia sheria za barabarani ili kuweza kupunguza ajali  pia jeshi hilo limetoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kupoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu amesema hadi kufika leo Disemba 18, 2024 Jumla ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo ni 15 na majeruhi 7 huku hali za majeruhi hao  zikiendelea vizuri kwa kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

Pia amesema Hadi kufikia leo  Disemba 18, 2024 miili ya watu watano kati ya 15 tayari ilikuwa imetambuliwa na ndugu zao, huku zoezi la kutambua miili iliyobaki likiendelea kwa siku 14 na baada ya muda huo ambao watakuwa hawajatambuliwa, hatua za kuwasitiri wapendwa hao litafanyika kwa mujibu wa taratibu za kiserikali.


Katika ajali hiyo madereva wote wawili walifariki dunia.


MWISHO.




Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.