• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

VIONGOZI WA DINI MOROGORO WASHAURIWA KUWA MABALOZI WA AMANI

Posted on: November 17th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amewataka Viongozi wa dini katika Mkoa huo kuwa mabalozi wa amani kwa kuwa wao wanaushawishi na nguvu kubwa katika kuwabadilisha waumini wao kitabia kupitia mafundisho wanayoyatoa kwenye nyumba zao za ibada.

Mhe. Fatma Mwassa ametoa kauli hiyo Novemba 16 mwaka huu wakati akifungua kikao cha kawaida cha Kamati ya Afya ya Msingi kwa Jamii kilichohusisha wataalamu wa Sekta ya Afya Pamoja na Viongozi mbalimbali wa dini Mkoani humo.

Mhe. Fatma Abubakar Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akifungua kikao hicho.

Mhe. Fatma Mwassa amewaomba viongozi hao wa dini kutoa Elimu kwa waumini wao kuacha kujichukulia Sheria mikononi lakini pia kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapoona kuna uvunjifu wa amani, ukiukwaji wa Sheria, taratibu na kanuni Katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za uingizaji wa  makundi makubwa ya mifugo unaendelea sasa Mkoani humo jambo ambalo amesema linachangia uvunjifu wa amani.

Baadhi ya Viongozi wa Dini walioshiriki kikao cha Afya ya Msingi

“...kwahiyo tunawaomba leo viongozi wetu wa dini, tunajua nyinyi mnanguvu kubwa na maneno yenu yanaushawishi mkubwa, tunaomba mkatusaidie kuelimsha jamii...” amesema Mhe. Fatma Mwassa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa, amewataka viongozi hao kutoa Elimu kwa waumini wao juu ya mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha ukame katika maeneo mengi hapa nchini na duniani kwa ujumla na kwqmba hali hiyo imechangiwa vikubwa na shughuli za kibinadam kama ukataji miti hovyo, uchomaji moto misitu, kuharibu vyanzo vya maji na shughuli nyingine zinazofanana na hizo, na kutaka kuwa mabalozi wazuri  kukemea matendo hayo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dr. Mussa Ali Mussa akiongea na viongozi wa dini na wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi ya Jamii waliohudhuria kikao hicho.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa dini kuelimisha waumini wao kupata chanjo ya uhonjwa wa Uviko 19 na chanjo za magonjwa mengine Kama surua na polio ili kuiweka jamii salama kiafya.

Kwa upande wake Shekhe mkuu wa Mkoa wa Morogoro Shekhe Twaha Kilango ameshauri viongozi wa Serikali kutumia zaidi busara zao Katika kutatua migongano ndani ya jamii ikiwemo Ile ya baina ya  wakulima na wafugaji, kwa kuwa nguvu pekee inaweza kuleta madhara makubwa lakini pia isilete Suluhu ya kudumu ya tatizo husika.

Sambamba na ushauri huo amewataka viongozi wenzake wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha waumini juu ya masuala ya amani na na masuala ya afya.

Naye Mhasham Askofu Jacob Mameo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT Dayosisi ya Mashariki amesema wapo tayari kwenda kukutana na makundi yote mawili ya jamii ya wafugaji na wakulima kwa lengo la kuwatuliza waache vurugu ambazo uwenda zinasababisha balaa la kutonyesha kwa mvua na mabalaa mengine.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Kusirye Ukio

Akitoa tathmini ya utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO - 19 Mkoani humo Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Morogoro Dkt. Masumbuko Igembye amesema toka Agosti 2, 2021, hadi Oktoba 31, 2022, takribani watu 1,022,093 sawa na 66.2% wamechanjwa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo huku lengo likiwa ni kutoa chanjo kwa watu 1,544,177 Mkoani humo.

Aidha, Dkt. Masumbuko amewataka viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kuchanja ili kufikia lengo la asilimia 80 hali itakayoleta matumaini ya mkoa huo kuwa salama dhidi ya ugonjwa wa COVID - 19.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.