• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Viongozi wa TAGCO wakamilisha ziara ya kikazi Mkoani Morogoro, watoa tathmini.

Posted on: August 31st, 2021

Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini - TAGCO kimewataka Maafisa habari hapa nchini kuiga mfano wa vitengo vya habari vinavyofanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao kikiwemo Kitengo cha Habari cha Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuwahabarisha wananchi juu ya shughuli  mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yameelezwa na Mjumbe Mtendaji wa TAGCO Bw. Karim Meshack Agosti 30 mwaka huu kwa niaba ya Wajumbe wenzake wakati wa ziara ya Uongozi wa Chama hicho wakishirikiana na Maafisa Habari Waandamizi kutoka Idara ya Habari Maelezo walipotembelea Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Baadhi ya Viongozi wa TAGCO waliofanya ziara Mkoani Morogoro. kutoka kushoto ni Karim Meshack, Gerlad Chami ambaye alikuwa Mkuu wa Msafara katika ziara hiyo na Fred Mwanjala ambaye  pia ni Afisa Habari Mwandamizi Idara ya Habari Maelezo.

Bw. Gerlad Chami akiwasilisha ujumbe wa TAGCO kwa Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakati wa kikao 

Bw. Meshack amebainisha kuwa, katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mkoa huo, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ndiyo imekidhi hadhi ya kuwa kitengo cha habari katika utekelezaji wa majukumu yake kutokana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kumwezesha Afisa habari kuwa na Maafisa habari wasaidizi watano ambao wanasaidia kuwapasha habari wananchi kwa wakati.

‘’Kitu kikubwa zaidi ambacho kimetufurahisha katika Manispaa ya Morogoro ni Mkurugenzi kumuwezesha Afisa habari kuwa na Maafisa wengine wa habari watano  ili kuhakikisha taarifa za utendaji kazi za Manispaa zinawafikia wananchi kwa wakati’’ amesema Meshack.

‘’kazi nyingi zinafanyika vizuri za kutangaza Manispaa na Mkoa kwa ujumla kutokana na uwepo wa Maafisa habari wa kutosha, tunaona namna ambavyo wanauza vivutio vilivyomo katika manispaa ya Morogoro ikiwemo stendi ya kisasa, soko, water falls na mambo mengine’’ ameongezea Meshack.

Katika hatua nyingine, Meshack  amebainisha kuwa Maafisa habari wa taasisi ni wasemaji na wawakilishi wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  katika kufikisha taarifa mbalimbali zinazotekelezwa katika Halmashauri au Mkoa husika.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya morogoro  Bi. Pilly Kitwana, pamoja na kushukuru ujio wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini-TAGCO, amesema ujio wao umesaidia kutambua mapungufu machache waliyo nayo hususan ya kutomtumia vyema Afisa Habari wa Halmashauri hiyo.

Aidha, ametumia fursa hiyo kumtaka Afisa Habari wa Halmashauri kuongeza juhudi katika kutangaza kazi zinazofanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Serikali kwa ujumla pamoja na kutangaza vivutio vyote vinavyopatikana ndani ya Halmashauri ya Manisapaa ya Morogoro.   

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Pilly Kitwana

Kwa upande wake Afisa habari wa Mkoa wa Morogoro Ndg. Andrew Chimesela amesema ujio wa TAGCO katika Mkoa huo umelenga kutathmini utendaji kazi wa Maafisa habari, kutoa ushauri na kuangalia namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa Habari wa Halmashauri za Mkoa huo.

Aidha, Bw. Chimesela amewapongeza Viongozi wa TAGCO kwa kuanzisha utaratibu wa kuwatembelea Maafisa wa habari kwa lengo la kujua changamoto zao na kuzitatua jambo ambalo amesema utamaduni huo unafaa uendelee ili kuleta mafanikio chanya ya Tasnaia ya Habari.

Naye, Afisa habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bi. Lilian Henry licha ya kuipongeza TAGCO, amesema ziara hiyo ya Wajumbe wa chama cha TAGCO imewatia moyo katika kukabiliana na changamoto ambazo Maafisa habari wanakumbana nazo hivyo kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi.

Lilian Henry Afisa Habari Manispaa ya Morogoro

Mkuu wa Kitengo cha ICT Manispaa ya Morogoro, Bw. Kitutu Mshana

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.