• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Vituo vya Afya, Zahanati kuanza kutoa huduma Januari 29, 2024.

Posted on: January 27th, 2024

Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ameziagiza Timu za Uendeshaji wa huduma za Afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri (RHMT na CHMT) nchini kuhakikisha kuwa Vituo vya Afya na Zahanati  ambavyo ujenzi wake umekamilika vianze kutoa huduma za awali kwa wananchi wa maeneo husika kuanzia Januari 29 mwaka huu.

Dkt. Mfaume ametoa agizo hilo Januari 27 mwaka huu wakati akizungumza na Watumishi wa Afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri Mkoani Morogoro wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya kukagua na kuangalia ubora wa huduma za Afya Mkoani humo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa Serikali imetoa fedha za ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya pamoja na Hospitali za Wilaya hapa nchini ambapo kwa asilimia kubwa ujenzi huo umekamilika lakini huduma hazijaanza kutolewa hivyo wamezitaka Timu hizo kuhakikisha huduma za awali zikiwemo za OPD, upimaji, huduma za mama na mtoto na upasuaji zianze kutolewa ifikapo Januari 29 mwaka huu.

"...naagiza na haya ni maagizo yangu kwa CHMT na RHMT nchi nzima zile huduma za awali ambazo majengo yake yamekamilika zianze kutolewa Januari 29...amesema Dkt. Mfaume.

Aidha, amezitaka timu hizo kusimamia Vifaa tiba vinavyopelekwa katika vituo vyao na kuhakikisha kuwa vinatunzwa na kutumika kama ilivyokusudiwa huku akiwataka kujiepusha na wizi wa vifaa hivyo na kwamba Serikali haitamfumbia macho mtumishi yeyote atakayebainika kufanya ubadhirifu wa vifaa tiba.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mfaume amewataka Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo yao hususan kipindi hiki cha mvua nyingi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kusirye Ukio amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa ziara yake huku akimuhakikishia kuwa maoni, maelekezo na maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake na wakati wa majumuisho watayafanyia kazi ili huduma za Afya Mkoani humo ziimarike.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Mziha akiwemo Bi. Angela Chengula ameishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajengea kituo cha Afya ambacho kimejengwa kupitia fedha za Tozo za miamala ya simu Shilingi milioni 500 na kwamba kituo hicho kinaenda kuwaondolea adha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 60 kufuata huduma za Afya.

Mkurugenzi huyo wa Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii amefanya ziara ya siku tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mvomero na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo alikagua ujenzi wa Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.