• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Vyama vya ushirika vyatakiwa kutumia TEHAMA katika utendaji kazi wake.

Posted on: May 18th, 2023

Vyama vya ushirika hapa nchini vimeshauriwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa shughuli zake za kila siku ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kurahisisha kuongeza ufanisi wa kazi katika utendaji wa vyama hivyo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa Mei 17 mwaka huu wakati akifungua mafunzo ya ya usimamizi kwa Maafisa wa vyama vya ushirika wa kanda ya mashariki inayojumuisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro yaliyofanyika katika hoteli ya Savoy Mkoani Morogoro.

Dkt. Mussa amebainisha kuwa ili vyama vya ushirika viweze kujiendesha kibiashara ni wazi suala la TEHAMA kwao halikwepeki na linatakiwa kuwekewa mkazo wa hali ya juu lengo likiwa ni kuondoa dosari ndogo ndogo zinazojitokeza mara kwa mara katika vyama vya Ushirika, hivyo kutojiendesha kibiashsara.

“...tuhakikishe tunatumia ipasavyo tehama, dunia inaendelea na teknolojia inakua kwa kasi, na kwa hakika ikituacha nyuma hakuna kitu kitakachoendelea... kwa hiyo kuna haja ya kuhakikisha kuwa Tume ya maendeleo ya ushirika na vyama vya ushirika vinakuwa na matumizi ya kiwango kikubwa cha Tehama...” amesema Dkt. Mussa.

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa akizungumza na washiriki wa mafunzo ya usimamizi kwa maafisa wa vyama vya ushirika wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Akibainisha Changamoto za Vyama hivyo amesema kuna ukosefu wa maadili na uadilifu miongoni mwa viongozi wa vyama hivyo na kushindwa kufikia ndoto waliyo nayo wakulima waliojiunga na vyama vya ushirika.

Katika Hatua nyingine Katibu Tawala huyo ameiagiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)kuhakikisha Tume hiyo inafanya kazi kwa karibu na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuondoa migogoro ya mara kwa mara inayojitokeza kwenye vyama vya Ushirika na kuboresha maisha ya wananchi wa chini ambao ndio walengwa namba moja wa vyama hivyo.

picha mbalimbali za Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa akiwa pamoja na viongozi wa Tume ya maendeleo ya vyama vya ushirika, wawezeshaji na washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika.

Aidha, Dkt. Mussa amesema mafunzo hayo yatarudisha imani ya wanaushirika katika vyama vyao kwa kuwa kuna mfumo mpya wa teknolojia wa uendeshaji wa vyama hivyo na kuongeza kuwa maafisa ushirika wajengewe uwezo wa uendeshaji wa vyama pamoja na kuwataka kuwa waadilifu katika kazi zao.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro Ndg. Solomon Kasaba amesema wanatarajia kuona mabadiliko ya uendeshaji wa vyama vya Ushirika na kwamba haitaleta maana kama pamoja na kupata mafunzo hayo bado ushirika utajiendesha kizamani.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Hussein Mohamed amesema ili kufikia Malengo ya Serikali kupitia sekta ya kilimo katika kuchangia fedha za kigeni Bilioni Tano na ajira Bil. Tatu kwa wananchi hasa vijana ifikapo mwaka 2030 ni lazima kuboresha vyama vya ushirika viwe Bora zaidi.

Akielezea faida za vyama vya ushirika Mrajisi na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika TCDC Dkt. Benson Ndiege amesema, mfumo wa kuuza mazao ya kimkakati kupitia vyama vya ushirika una manufaa makubwa tofauti na kuuza mazao hayo kwa mkulima mmoja mmoja.

Akibainisha hayo Dkt. Benson amesema kwa mfano msimu wa kilimo 2021/2022 na 2022/2023 zaidi ya tani trilioni 1.009 za mazao ya kimkakati ikiwemo tumbaku, kahawa, korosho pamba na mkonge ziliuzwa kupitia vyama vya ushirika ambapo zaidi ya Tsh. trilioni 2.9 zilipatikana, kati ya fedha hizo shilingi bilioni 15.144 zilikusanywa kama ushuru kupitia mamlaka za Serikali za mitaa.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.