• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Wadau wa Maendeleo Mkoani Morogoro waombwa kuchangia programu ya MMMAM

Posted on: September 7th, 2023

Utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT – MMMAM) katika jamii unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa Rasilimali watu na fedha, hivyo kufanya kasi ya usambazaji wa uelewa wa programu hiyo kusuasua, hivyo wadau wa maendeleo hususan Sekta binafsi wameombwa kuchangia katika utekelezaji wa programu hiyo.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Rasilimali watu na Utawala Bw. Herman Tesha akizungumza na wadau wa maendeleo wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha wadau wa malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Hayo yamebainishwa Septemba 06 mwaka huu na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Rasilimali watu na Utawala Bw. Herman Tesha wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha wadau wa malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto kilichofanyika  katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Bw. Tesha amesema pamoja na serikali kufanya jitihada za kuiendeleza programu hiyo lakini bado kunachangamoto ya rasilimali watu na fedha hivyo wadau wa maendeleo wanamchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa jamii inapata uelewa wa kutosha, hivyo amewaomba wadau hao kuchangia katika utatuzi wa changamoto hizo.

“...lakini niwaombe sana wadau wote ambao tumeshiriki hapa na wale ambao hawapo hapa kuendelea kuchangia kwa hali na mali kwenye utekelezaji wa programu hii...” amesema Bw. Tesha.

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo amebainisha kuwa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 imeonesha asilimia 30 ya watoto Mkoani humo wanaudumavu, asilimia 10 wanauzito pungufu na asilimia 3.9 wanaukondefu hivyo jamii imeshauriwa kupitia programu hiyo kuzingatia lishe bora.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Rasilimali watu na Utawala Bw. Herman Tesha akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo baada ya ufunguzi wa  kikao kazi cha siku moja cha wadau wa malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuweka msukumo katika utekelezaji wa programu hiyo ikiwemo kuboresha huduma za afya hususan za mama na mtoto pamoja na kuboresha sekta ya elimu  kuanzia ngazi ya awali kwa kujenga madarasa.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Childhood Development Organization Bi. Felistas Kalomo amewasisitiza wadau hao kuchangia utekelezaji wa programu hiyo ili kupata matokeo chanya yanayotarajiwa.

Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Childhood Development Organization Bi. Felistas Kalomo akisisitiza wadau wa maendeleo kuchangia utekelezaji wa programu ya MMMAM.

Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT – MMMAM) imelenga kuhamasisha Afya bora kwa mama na mtoto, lishe bora, malezi yenye muitikio, ulinzi na usalama wa mtoto pamoja na fursa za ujifunzaji kwa watoto walio kati ya miaka 0 hadi 8 na inatekelezwa ndani ya miaka mitano 2021 hadi 2026.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.