• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI LUKUVI ATOA MIEZI MIWILI.

Posted on: June 8th, 2021

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  amewataka Makamishna wa Ardhi nchini kufanya upekuzi wa mashamba yaliyomilikishwa katika maeneo yao ili wasio yaendeleza wachukuliwe hatua za kubatilisha miliki zao kisha kupewa watu wengine.

Mhe. Lukuvi ametoa agizo hilo Juni 8, mwaka huu  wakati wa ziara yake Wilayani humo iliyolenga kurejesha mashamba  hayo kwa wananchi yaliyobatilishwa na Serikali baada ya kuona hayaendelezwi.

‘’Makamishna wa Ardhi wa Mikoa yote hakikisheni mnafanya upekuzi  wa mashamba yote yaliyomilikishwa katika maeneo yenu ya Mikoa ili wale wasiyoyaendeleza hatua za kisheria zichukuliwe za kubatilisha miliki ili wapewe watu wengine’’ Amesema Mhe. Lukuvi.

Aidha, Mhe. Lukuvi amesema kuna mashamba mengi nchini ambayo hayaendelezwi hali ya kuwa kuna idadi kubwa ya wananchi ambao wanahitajio la mashamba hayo kwa ajili kufanya shughuli mbalimbali za kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa jumla.

Sambamba na hayo, Mhe. Lukuvi ametoa miezi miwili kwa  Maafisa Ardhi Wilayani Mvomero kufanya upekuzi wa mashamba 86 yaliyotelekezwa na wamiliki wake ili yawasilishwe kwenye mamlaka husika kwa lengo la kufutwa na kurejeshwa kwa wananchi.

‘’Nataka haya mashamba 86 ambayo tunaamini kwamba hayaendelezwi vizuri yafanyiwe upekuzi haraka ili tujue yale ambayo hayafanyiwi kazi vizuri tupeleke kwa mamlaka hatua zichukuliwe, yafutwe ili wananchi wengine wanaotaka kuendeleza Ardhi hiyo kwa faida waweze kuyaendeleza’’.

‘’Hatuwezi kuacha wananchi wanabanana hawana Ardhi ya kutumia lakini kuna watu wana mashamba 86 hapa yamepimwa hayalipiwi kodi ya Ardhi, hawayaendelezi halafu wanasababisha uvamizi’’ Amesema Mhe. Lukuvi

Pia, Mhe. Lukuvi amesema mashamba 9 yenye hekari 13, 900.5 yamefutwa katika Kijiji cha Wami Luhindo ambapo hekari 9, 700 kati  hizo watapewa wananchi na 4,100 zinazobaki zitatengwa kwa ajili ya wawekezaji ambao watakuwa wanalipa kodi kupitia mashamba hayo, hali ambayo itasaidia kukua kwa uchumi katika Wilaya hiyo..

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela, amewataka wanachi na watendaji wa Serikali Wilayani humo kutekeleza maagizo ya Mhe.Waziri Lukuvi ili migogoro ya Ardhi iweze kupungua ama kuisha kabisa katika Wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine, Mhe.  Shigela amewataka watendaji ngazi ya Vijiji kuzingatia sheria ya umiliki wa Ardhi na sheria ya kupanga matumizi ya Ardhi kwa lengo la kutokuwa chanzo cha migogoro kwa wananchi wanapohitaji Ardhi kwa ajili ya matumizi ya shughuli za maendeleo.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.