• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI MKUCHIKA ATOA MAELEKEZO KWA WAZAZI NA WALEZI NCHINI.

Posted on: October 27th, 2024



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum) Mhe. George Mkuchika amewataka wazazi na walezi hapa nchini kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni ili kuweza kujua changamoto  zinazowakabili na kuzitatua ili kuweza kuongeza ufaulu mashuleni.

Waziri huyo amesema hayo Oktoba 26, 2024 wakati akikagua ujenzi wa bweni na kuzindua madarasa mapya katika shule ya Sekondari Kingolwira iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema  ni wajibu  wa wazazi na walezi kushirikiana na kamati za elimu za shule za Msingi na Sekondari kuhakikisha wanafuatilia watoto wao pindi wanapokuwa shuleni ili kuweza kuwasahihisha pale wanapokosea na kuweza kuongeza ufaulu wao mashuleni.

"..Wazazi wenzangu hakikisheni mnafuatilia maendeleo ya watoto wenu mashuleni.." amesisitiza Mhe. George Mkuchika

Pia Mhe. Mkuchika amewapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuufanya Mkoa kuwa namba 3 katika uandikishaji hivyo amewataka wananchi hao kufanya kampeni za kistaarabu.

Katika hatua nyingine Mhe. Mkuchika amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea  kuweka jitihada kubwa katika kuhakikisha changamoto katika Sekta ya Elimu zinaepukika hapa nchini na kuwapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kutumia mapato ya ndani kujenga na kusimamia miradi na kuwaletea wananchi maendeleo.

Sambamba na hayo, Mhe. Mkuchika amesema hakuna nchi inayoendelea bila kuwepo kwa amani na upendo hivyo ni jukumu la kila Raia wa Tanzania kuhakikisha wanatunza amani na upendo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu ya nane choo pia ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Kingolwira ambapo wanatarajia kuanzisha kitado cha tano na sita katika shule hiyo na kwenda kuondoa changamoto ya uhaba wa shule za (Advance level) katika Halmashauri hiyo.

Naye Bi. Shangwe Mose Mkuu wa Shule ya Sekondari Kingolwira amesema ujenzi wa madarasa 4 na matundu 8 ya vyoo umeanza Aprili 15, 2024 na kukamilika Agosti 8, 2024 ambapo mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 102 na laki nne pamoja na matengenezo ya viti na meza160.

Mhe. Mkuchika amezindua madarasa manne na matundu nane ya vyoo shule ya Sekondari Kingolwira, ametembelea ujenzi wa bweni  la wanafunzi shule ya Sekondari Kingolwira, ametembelea ujenzi wa barabara ya (TACTIC) amekagua ujenzi wa Hopsitali ya Wilaya na kuzindua zahanati ya Mji Mpya ambapo miradi hiyo ipo katika  Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.