• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI SILAA ATATUA MIGOGORO MKOANI MOROGORO

Posted on: July 9th, 2024

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (MB) ametatua migogoro ya Ardhi ya muda mrefu likiwemo eneo la Msitu wa kuni - CCT baada ya wananchi  kuvamia eneo hilo na kuweka makazi yao ya kudumu ambapo Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassani alitoa maelekezo juu ya kupimwa eneo hilo na kuwapatia wananchi umiliki halali.

Makubaliano hayo yamefikiwa Julai 9, mwaka huu baada ya Waziri Jerry Silaa kuwasili Wilayani Mvomero na kufanya mkutano na  wananchi waliovamia  eneo hilo.

Akibainisha zaidi katika mgogoro huo wa Msitu wa kuni Waziri Silaa amesema, Dkt. Samia Suluhuhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kutoa Ekari 5113 kutoka katika msitu huo na kupima Viwanja 1204 ambavyo wananchi waliokuwa wakiishi humo watahakikiwa na kupewa hati za umiliki. 

"... Rais Samia kaagiza ekari 5113 zimegwe kwenye msitu wa Watanzania na eneo hilo lipimwe viwanja 1204 na hivyo viwanja vitatolewa vibali kwa utaratibu mzuri uliopangwa..." amesema Mhe. Jerry Silaa. 

Katika hatua nyingine, Waziri Jerry Silaa amesema Serikali imeridhia kutoa hati miliki za ardhi kwa wananchi walipatiwa maeneo eneo la Msamvu tangu 1978 na kuanzisha makazi ya kudumu na biashara licha ya ramani ya awali iliyoonesha eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya  shughuli nyingine za kijamii ikiwemo viwanja vya michezo.

Pia amesema kwa sasa serikali haitatoa vibali vya kumilikisha maeneo ya wazi bali ramani itabaki kama ilivyo na kutaka watendaji wa sekta ya Ardhi hapa nchini  kuhakikisha maeneo yenye migogoro kusikilizwa na kumalizika ili kuepuka kuiingiza serikali kwenye migogoro isiyo na tija.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amempongeza Waziri Jerry Silaa kwa kutenga muda wake kwa ajili ya kutatua kero za wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususan zinazohusu migogoro ya Ardhi.

Hapo awali, Kamishna Msaidizi wa ardhi Mkoa wa Morogoro Bw. Frank John Minzikuntwe amesema Mwaka 2022 Serikali ilitoa maelekezo ya kuwahakiki wananchi waliokuwa wamejenga nyumba zao eneo la Msitu wa kuni na baada ya upimaji wa ekari 5113 vimepatikana viwanja 1204 ambavyo vitapewa hati miliki huku maeneo ya wazi yatabaki serikalini.

Nao wananchi akiwemo Bi. Chiku Ramadhani Mgangu Mkazi wa Mianga ameishukuru Serikali kwa kuendesha zoezi la kupimiwa viwanja na kuhakikiwa maeneo yao na kupewa vibali kwa ajili kupewa hatimiliki.


 


Mwisho.


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.