• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUSHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Posted on: February 14th, 2025


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka  wananchi wa Mkoa huo kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambapo kwa Mkoa wa Morogoro kilele cha maadhimisho hayo ni Machi 8, 2025 katika Wilaya ya Kilombero yakiambatana na kaulimbiu isemayo "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji."

RC Adam Malima ametoa wito huo leo Februari 14, 2025 wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo huku akiwataka wananchi wote kutumia fursa hiyo kumwezi Mheshimiwa Rais pamoja wa wanawake vinara katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wananchi.


Aidha, amesema katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ni wajibu wa wanamorogoro wote kushiriki kikamilifu ili kuungana kwa pamoja kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu, huku wakitambua mchango wa wanawake na wasichana katika maendeleo ya Taifa letu.


"..Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro kushiriki kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.." Amesema Mhe. Adam Malima.


Sambamba na hayo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika maadhimisho hayo ngazi ya Mkoa yataanza kufanyika Machi 6, 2025 ambapo kutakuwa na Shughuli za utalii, zitakazotoa fursa ya kujifunza na kuona vivutio vya utalii vilivyoko ndani ya mkoa huo na

Machi 7, 2025 kutakuwa na Kutoa msaada kwa wahitaji, Semina, Maonesho na Usiku wa Mwanamke.


Sanjari na hayo Mhe. Malima amesema kwa ngazi za Halmashauri maadhimisho hayo yataanza Machi 1- 5, 2025 ambapo yataambatana na matukio mbalimbali yakiwemo, Kuandaa mahojiano kuhusu nafasi ya mwanamke na mchango wake, kuandaa maonesho ya vikundi vya wanawake wajasiriamali, kuandaa makongamano yanayobeba ujumbe wa kauli mbiu, kuzindua afua/miradi mbalimbali ya kijamii na kutoa tuzo kwa wanawake vinara.


Shughuli nyingine zitakazofanyika wiki hiyo ni pamoja na kuandaa usiku wa mwanamke, kuendesha mashindano ya kitaaluma na michezo kutoa misaada ya kijamii kwa makundi ya wahitaji, kuandaa matembezi ya hiari na mashindano ya michezo, kuendesha kliniki ya msaada wa kisheria, bonanza la michezo kwa timu za wanawake na kushiriki kufanya shughuli mbalimbali za miradi ya kijamii.


Katika hatua nyingine Mhe. Malima  amewataka Wakuu wote wa Wilaya za Mkoa huo kusimamia kikamilifu maandalizi ya maadhimisho hayo na kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli zote zilizopangwa kufanyika  kama ambavyo Wizara imeelekeza.


Katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa Mkoa wa Morogoro mgeni rasmi wa maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mhe. Adam Kighoma Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.