Rais Mstaafu wa awamu ya nne (4) Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema reli ya kisasa ya mwendokasi (SGR) itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa haraka kwa kuiingizia Serikali mapato yatakayotokana na wasafiri na usafirishaji hivyo amesema hatuna budi kuilinda na kuitunza kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Dkt. Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Julai 24, 2024 alipowasili katika kituo cha Reli hiyo cha Mkoni Morogoro baada ya kutumia usafiri huo akitokea Dar es Salaam akiambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima na viongozi wengine wa Serikali akiwemo Mkurugenzi Mkuu TRC Masanja Kungu Kadogosa.
MWISHO.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.