• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Kamati ya Siasa Morogoro haijaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Mbingu.

Posted on: October 1st, 2024

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya  CCM Mkoa  wa Morogoro imesema haijaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa barabara ya Ifakara - Mbingu Wilayani Kilombero uliotakiwa kuanza rasmi kutekelezwa Disemba 8, 2023 lakini hadi sasa bado unasuasua.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 29, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi Joseph Masunga kwa niaba ya wajumbe wenzake baada ya kutembelea mradi huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yao ya siku tano kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho mkoani humo.

"...nieleze masikitiko yangu kutokana na mradi huu kususasua... barabara ndio kero kubwa katika maeneo ya huku..." amesema Mhandisi Joseph Masunga. 

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imeelezwa kuwa changamoto kubwa ya mradi huo ni mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kutolipwa malipo ya awali (Advance Payment) ambayo kimsingi ni haki yake kwa mujibu wa mkataba huo.

Kwa sababu hiyo, Mhandisi Masunga ameiagiza Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa kufuatilia kwa karibu changamoto hiyo na ili mkandarasi huyo alipwe na kuanza mara moja kwani amesema adha kubwa ya wananchi wa Mlimba ni uwepo wa ubovu wa barabara hususan wakati wa masika.

Hata hivyo, Mhandisi Masunga ameipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye sekta ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mlimba na kutumia fursa hiyo kuwapongeza watendaji wote wa serikali ngazi ya Mkoa, Wilaya na ngazi nyingine kwa kusimamia maono ya Rais. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima, amesema mradi wa Barabara ya Ifakara - Mbingu uko mikononi mwa TANROADS Makao Makuu na Mkoa hivyo ametaka kujipanga zaidi ili kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa mapema kwa manufaa ya taifa na usafirishaji wa mazao ya wananchi.


Naye Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Bw. Geofrey Mtakubwa amesema, mpaka sasa kazi  zilizofanyika katika mradi huo ni upimaji, ujenzi wa kambi ya mkandarasi na kuleta vifaa 57 kati ya 137 ambapo ni sawa na 41.6% pamoja na kuleta wataalamu 7 kati ya 9 wanaohitajika.

Barabara hiyo yenye urefu wa km 62.5, inayojengwa kwa kiwango cha lami itakayogharimu shilingi Bil.97.1 inatekelezwa na mkandarasi M/S Henan Highway Engineering Group ya nchini China na kusimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ulitakiwa kuanza kutekelezwa Disemba 8, 2023 na kukamilika Juni 8 ,2026.

Mwisho

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.